NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, MHESHIMIWA MARY MASANJA AELEZA UMUHIMU WA BONDE LA KILOMBERO

Na John Bera-WMU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amesema Bonde la Pori Tengefu la Kilombero ni sehemu ya ardhioevu linalochangia asilimia 62.5 ya maji yote ya mto rufiji hivyo kuwa chanzo muhimu cha maji kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akijibu swali Bungeni jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine amesema Bonde la Pori tengefu la Mto Kilombero ni muhimu Kitaifa na Kimataifa kutokana na uhifadhi wa bionuwai zilizo adimu Duniani kama vile mnyama aina ya sheshe. (Picha na John Bera-WMU).

Amesema Bonde hilo lina umuhimu kitaifa na Kimataifa kutokana na uhifadhi wa bionuwai zilizo adimu Duniani kama vile mnyama aina ya sheshe.Maji ndio muhimili wa

Kutokana na maji yaliyopo kwa wingi huwa yanawezesha wanyamapori kama sheshe ambao hutegemea ardhi chepechepe kuendelea kuishi muda mrefu.

Ripoti zinaonesha kuwa, Bonde la Kilombero ambalo lilitengwa kuwa Pori Tengefu kwa Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Sura ya 302 ya mwaka 1952 (Fauna Conservation Ordinance CAP 302 
of 1952 GN.No.107) likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 6,500 na kurithiwa na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori No. 12 ya mwaka 1974 lina historia ndefu.

Aidha,Serikali ilitenga bonde hilo kuwa Pori Tengefu tena kwa Tangazo la Serikali Namba 459 la mwaka 1997.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news