Wadau wamuunga mkono Rais Samia michezo ya Olimpiki

Na John Mapepele, Mtwara

Mdau wa michezo nchini, Kampuni ya Ocean Silent Ltd, amesema anajitolea vyakula kwa ajili ya kuisaidia timu ya riadha katika kipindi chote kilichobaki wakati timu hiyo inapojiandaa kushiriki mashindano ya Olympic yanayotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2021 katika jiji la Tokyo nchini Japan ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu katika kuinua michezo hapa nchini.

Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni hiyo Bwana Muhamed amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia inafanya kazi nzuri katika kuleta mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Michezo,Sanaa na Utamaduni hivyo ni wajibu wa kila mdau kuunga mkono ili sekta hizo ziweze kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa.

Akipokea msaada vyakula hivyo vilivyogharimu milioni 3,5 mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo amewashukuru wadau hao kwa kuiunga mkono Serikali katika juhudi za kukuza na kuendeleza michezo nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo (aliyeshika mfuko) kwenye picha ya pamoja na timu ya riadha na wafanyakazi ya Kampuni ya Ocean Silent Limited baada ya kukabidhiwa msaada wa vyakula.

Mkurugenzi Singo amefafanua kwamba kambi ya maandalizi ya wanamichezo kwa ajili ya mashindano hayo inaendelea vizuri mkoani Arusha na timu ya wanamichezo hao inatarajiwa kuondoka nchini Juni 29, 2021 ambapo inahusisha wanamichezo watatu ambao wamefuzu na kufikia viwango vya mashindano hayo.

Amesema pia wapo wachezaji wengine wawili ambao wamefuzu kushiriki Olympic maalum Paraolympic kwa wachezaji wenye ulemavu watakaoshiriki mapema mwezi wa nane.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo akiongea na Vyombo vya Habari akiwataka wadau wa michezo kuendeleza vipaji vya wanamichezo kuanzia kwenye mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA.

Ushiriki wa Kampuni ya Ocean Silent Ltd katika kufanikisha kambi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 ikiwa inawataka wadau kushiriki pamoja na serikali katika kuleta maendeleo katika michezo.

Amesema mkakati wa serikali kwa sasa ni kuhakikisha michezo kuanzia ngazi za chini hadi taifa ambapo amesema ni kutokana na mikakati hiyo mwaka huu Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayoendelea mjini Mtwara yameratibiwa na Wizara tatu za Habari, Elimu na TAMISEMI ili yaweze kuwa na tija kuliko awali.
Wanariadha wakijipanga kwa ajili ya kushiriki mbio za mita 1500 kwenye mashindano ya UMITASHUMTA yanayoendelea mjini Mtwara yaliyofunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Juni 8, 2021.

Amewataka wadau kujitokeza kuja kuangalia vipaji vya wanafunzi katika mashindano haya ili kwa kushirikiana na Serikali waweze kuwaendeleza.

Ameongeza kuwa, kauli mbiu ya mashindano hayo ya mwaka huu inayosema “Michezo, Sanaa na Taaluma kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda” inasadifu kwa
kiasi kikubwa nia ya Serikali katika kuifanya michezo katika kiwango cha kimataifa ili ichangie kwenye uchumi wa nchi.

Pia amesema wanafunzi sita watakaofanya vizuri mashindano ya UMITASHUMTA upande wa Riadha yanayoendelea kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu mjini Mtwara watapelekwa katika mashindano ya kimataifa ya Shirikisho la Michezo ya Wanafunzi Duniani (ISSF) yatakayoanza Septemba mwaka huu nchini Slovenia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news