Wawili Mahakamani Dar kwa kumdanganya DPP Mwakitalu kuwa ni Usalama wa Taifa

Mfanyabiashara, Joshua Jelemia (37) na Yahaya Abdallah (31) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ya kujifanya Maofisa Usalama wa Taifa (TISS) katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na naibu mkurugenzi wa mashtaka, anaripoti MWANDISHI DIRAMAKINI.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani Juni 18, 2021 na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.

Akiwasomea shtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai wanadaiwa kutenda makosa hayo Juni 12, 2021 katika ofisi za DPP zilizopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani.

Inadaiwa siku hiyo wawili hao walijitambulisha kwa Slyvester Mwakitalu (DPP) na naibu wake (DDPP), Joseph Pande kuwa wao ni maofisa kutoka TISS.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na hivyo wapangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hoja za awali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, 2021 na washtakiwa kurudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.

Hii si picha kamili ya tukio hilo. (Picha na Mtandao).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news