Waziri Mwingulu awasilisha bajeti tamu kwa Watanzania

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasilisha Bungeni Makadirio ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022 huku ikianisha maeneo mbalimbali ya vipaumbele kwa mwaka huo wa fedha.

Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt.Mwigulu Nchemba amewsilisha hotuba hiyo leo Juni 10, 2021 bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2021/22.

Mheshimiwa Mwingulu amesema kuwa, bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. Bajeti hii itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali.

“Vipaumbele vilivyoainishwa katika maeneo matano ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22,Maeneo hayo ni Kuchochea uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu.

Waziri Mwigulu ameeleza kuwa ili kuwa na uchumi shindani na shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi ambayo itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi kwa ujumla.

Amefafanua kuwa, kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji,kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje na kuendeleza miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua fursa za kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini na barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani, mageuzi ya TEHAMA pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya Kidijitali, nishati, bandari na viwanja vya ndege. 

Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44 ikijumuisha shilingi trilioni 3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo.

Pamoja na mambo mengine ameitaja miradi mingine ya kielelezo itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Ruhudji MW 358.

“Mradi wa Kufua Umeme wa Maji – Rumakali MW 222; Uchimbaji wa madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi; Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na Mnazi Bay North; Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa Jamii; na kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi,"amesema.

Amesema kuwa, katika eneo la kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa kwenye miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za ugani;kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi; kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi; kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya kisasa na minada ya mifugo.

Mheshimiwa Mwingulu akisoma makadirio hayo ya bajeti akiwa ametumia saa 2:20,  ametaja maeneo mbalimbali ambayo bajeti hiyo imegusa ikiwemo maslahi ya watumishi, waendasha bodaboda, mikopo kwa elimu ya juu, kilimo na mengine mengi.
 
 Wafanyakazi

Mheshjimiwa Mwingulu amesema, Serikali inapendekeza kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira (PAYE) kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8.

Amesema, hatua hii ni mwendelezo wa juhudi za Serikali za kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi, ambapo kiwango hicho kimepunguzwa kutoka asilimia 11 mwaka 2015/16 hadi asilimia 8 itakayoanza kutekezwa mwaka 2021/22;

Aidha, amependekeza kufuta tozo ya asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention Fee) kwa wanufaika.
 
Pia amesema kwamba, anapendekeza Serikali kutenga sh. bilioni 449 kwa ajili ya kuwapandisha vyeo watumishi 92,619.

Vicheko kwa madiwani, maafisa tarafa, watendaji
 
Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato.

Kwa upande wa halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) amesema zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za madiwani kupitia kwenye akaunti zao.

Kwa upande wa Maafisa Tarafa amesema anapendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho ya sh. 100,000  kwa mwezi kwa kila Afisa Tarafa ili waweze kumudu gharama za mafuta na matengenezo ya pikipiki.

Kuhusu Watendaji Kata, amesema anapendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali kuanza kulipa posho ya sh. 100,000 kwa mwezi kwa kila Mtendaji Kata kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa yakitumika kulipa madiwani.
 
Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Akizungumzia madeni ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Waziri amesema, anapendekeza kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko kwa kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum isiyo taslimu (Non- cash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti kuanzia miaka miwili.

Kwa upande wa kuchelewa kwa michango ya watumishi kwenda kwenye mifuko, amesema, anapendekeza kulipa michango hiyo moja kwa moja kutokea Hazina kwa taasisi zote ambazo watumishi wanalipwa na Hazina.

Ameongeza kuwa, taasisi ambazo zinalipa watumishi kutokana na  vyanzo  vyao  vya  mapato  zitaendelea kufanya hivyo.
 
Jeshi la Polisi

Kuhusu Polisi, Waziri amesema anapendekeza kuanzia mwaka 2021/22 askari wa Jeshi la Polisi wataingia mkataba wa kipindi cha miaka sita na kuingia katika ajira ya kudumu badala ya miaka 12 ya awali. 
 
Kodi ya Majengo

Akizungumzia kodi ya majengo, Waziri Mwigulu amesema, Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ya majengo.
 
Kodi ya Wajasiliamali

Waziri Mwigulu amesema, TAMISEMI itaendelea na uratibu wa kugawa vitambulisho vya wajasiriamali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato  Tanzania ambayo ndiyo yenye mfumo wa kusajili.
 
Misamaha ya Kodi

Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kusamehe VAT kwenye madini na makinikia yatakayoingizwa nchini kwa ajili ya kuchenjuliwa, kuongezewa thamani na kuuzwa kwenye masoko ya madini.

Amependekeza kusamehe VAT kwenye huduma za bima ya mifugo ili kuchochea shughuli za ufugaji nchini;

Maeneo mengine ni kusamehe VAT kwenye bidhaa na huduma zitakazoingizwa au kununuliwa hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mafuta ghafi (EACOP), kusamehe VAT kwenye mafuta ghafi yanayotambulika kwa H.S Code 2709.00.00 kwa lengo la kutoa unafuu kwa mlaji ikiwemo Kampuni ya uendeshaji wa bomba la mafuta na kusamehe Kodi ya VAT kwenye nyasi bandia na maeneo mengine.
 
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147

Waziri Mwigulu amependekeza kufanya marekebisho ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zifuatazo:

BIA

Amesema, anapendekeza kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi 765 kwa lita za sasa hadi sh. 620 kwa lita. Lengo la mapendekezo haya ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini;
 
Mabasi ya elimu

Amesema, anapendekeza kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mabasi ya abiria yanayotambulika.
 
 Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82

Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kupandisha kiwango cha chini cha idadi ya waajiriwa wanaostahili kulipiwa kodi kutoka 4 wa sasa hadi 10. Lengo la marekebisho haya ni kuwapunguzia mzigo wa kodi waajiri wenye idadi ndogo ya waajiriwa na kuchochea ukuaji wa uwekezaji nchini;

Amesema, anapendekeza kufuta tozo ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa hospitali zinazomilikiwa na taasisi za kidini kwa kuwa taasisi hizi zimekuwa zikiisaidia sana Serikali kufikisha huduma za afya hata kwenye maeneo ambayo Serikali haijaweza kupeleka huduma kutokana na ufinyu wa bajeti.
 
Sheria ya Usajili wa Magari

Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usajili wa Magari SURA 124, kwa kupunguza ada ya usajili wa magari kwa namba binafsi kutoka sh. 10,000,000 hadi sh. 5,000,000 kila baada ya miaka mitatu.

Pikipiki
 
Waziri Mwigulu amesema, anapendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani SURA 168 kwa makosa ya Pikipiki na Bajaji kutoka sh. 30,000 za sasa hadi shilingi 10,000 kwa kosa moja.
 
Wanafunzi elimu ya Juu

Kwa upande wa elimu ya juu amesema, zaidi ya wanafunzi 11,000 wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu ambao tayari walishapata udahili katika vyuo mbalimbali walikosa mikopo.

"Naongelea mkopo, sio fedha ya bure, bali ni mkopo ambao ataurejesha. Katika jamii nyingi za kitanzania, mtoto akikosa mkopo huku akiwaona wenzake wanaendelea, inamfadhaisha sana.
 
"Ni mfadhaiko kwake na familia nzima. Kwa hatua ya maendeleo ambayo nchi yetu imepata katika sekta mbalimbali hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Serikali inakusudia kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa inaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwanufaisha vijana wote wenye sifa za kupata mkopo," amesema Mwigulu.

Sheria ya Petroli, SURA 392

Kwa upande wa sheria hiyo amesema, anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Petroli ili kuongeza tozo ya Mafuta ya Taa kutoka sh. 150 hadi sh. 250.

Amesema, lengo la hatua hii ni kupunguza uchakachuaji wa mafuta kufuatia ongezeko la ushuru wa mafuta kwenye dizeli na petroli.
 
Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki

Amesema, anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki kama ifuatavyo:

"Kutoza tozo ya sh. 10 hadi sh. 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14; na

"Mengine ni kutoza kiasi cha sh. 10 hadi sh. 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji.Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha sh. milioni 396,306,"amesema.
 
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa

Amesema, kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, anapendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya vinywaji vikali na bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.
 
Amesema, utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha sh. milioni 2,033,639.

Ameongeza kuwa,  hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo. 

Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).

Amesema, katika jitihada za kupanua wigo wa vyanzo vya rasilimali fedha, Serikali itaangalia uwezekano wa kutumia Hati Fungani zitakazotolewa na Halmashauri za Manispaa na Majiji kama njia mbadala ya kupata rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati.

Amesema  hatua hii itapunguza mzigo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali hasa kwa Halmashauri zenye miradi ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu na kuwa na uhakika wa uwezo wa miradi hii kujiendesha kwa faida (bankable projects).

"Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (United National Capital Development Fund - UNCDF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (Capital Markets and Securities Authority - CMSA) imeanza mchakato wa kuhakikisha kwamba Halmashauri, Manispaa na Majiji yatakayokidhi vigezo na masharti ya matumizi ya Hati Fungani hizi yanaanza kutumia utaratibu huu," amesema.

Kuhusu Zanzibar, Waziri amependekeza kufanya marekebisho ya Sheria  ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa  kurejesha VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na  kutumika Tanzania Zanzibar. Hii inatokana na mfumo wa  kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za  viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar  wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na  kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.

 Aidha, amependekeza marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa  zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa  bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara  sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za  VAT kwa pande zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa  marejesho, maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina  ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kutokana na utaratibu huu,  kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la Thamani  kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa. 

Amesema kuwa, kutokana na hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla  zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 55,499.97.

Kuhusu Sheria ya Kodi ya Mapato,Waziri amependekeza kufanya marekebisho  kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza Kodi ya Mapato  yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8. 

Waziri  amesema kuwa, jumla ya Mapato Kiwango cha Kodi sasa  

Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi  3,240,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  3,240,000/= lakini hayazidi  

shilingi.6,240,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  6,240,000/= lakini hayazidi shilingi  9,120,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  9,120,000/= lakini hayazidi shilingi  12,000,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  12,000,000/= 

Jedwali Na. 1B Viwango vinavyopendezwa

Mapato ya jumla yasiyozidi shilingi  3,240,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  3,240,000/= lakini hayazidi shilingi  6,240,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  6,240,000/= lakini hayazidi shilingi  9,120,000/=  

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  9,120,000/= lakini hayazidi shilingi  12,000,000/= 

Mapato ya Jumla yanayozidi shilingi  12,000,000/= 

Hakuna kodi 

9% ya kiasi kinachozidi shilingi  3,240,000/= 

Shilingi 270,000/= jumlisha 20% ya  kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/= 

Shilingi 846,000/= jumlisha 25% ya  kiasi kinachozidi shilingi 9,120,000/= 

Shilingi 1,566,000/= jumlisha 30% ya  kiasi kinachozidi shilingi  

12,000,000/= 

Hakuna kodi 

8% ya kiasi kinachozidi shilingi  3,240,000/= 

Shilingi 240,000/= jumlisha 20% ya  kiasi kinachozidi shilingi 6,240,000/= 

Shilingi 816,000/= plus 25% ya kiasi  kinachozidi shilingi 9,120,000/= 

Shilingi.1,536,000/= plus 30% ya  kiasi kinachozidi shilingi  

12,000,000/= 

Pia amesema kuwa, hatua hiyo inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda  mrefu kuwapunguzia mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii  inatarajiwa kupunguza mapato kwa shilingi milioni  14,178.06,kwa Kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye hatifungani za  Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi ya Mapato  kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la  hatua hii ni kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea kusaidia kugharamia miradi ya Serikali.

Amesema kuwa, kumekuwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka  kwa nchi wahisani zinazokwenda kutekeleza Miradi ya  maendeleo. Napendekeza Kurejesha utaratibu wa Mamlaka ya  Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha kwa kutoa  tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya Baraza  la Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili  kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali yenye kifungu kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato. 

‘’ Lengo la marekebisho haya ni kuharakisha utekelezaji wa  madi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo yenye gharama  nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa kusubiri  ridhaa ya Baraza la Mawaziri,’’amesema.

Amesema kuwa Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili kwenye  malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na  uvuvi yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika yote yanayojihusisha na usindikaji na ununuzi wa mazao,Kwa sasa, Taasisi za Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi  ya Chakula (NFRA) ndizo zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha  asilimia mbili.

 Aidha,amesema kuwa pendekezo hilo halitahusisha wakulima  wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko ya  msingi (AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni  kuweka usawa katika utozaji wa kodi kwa Kampuni zote zinazojishughulisha na mazao ya Kilimo, mifugo na uvuvi.Pendekezo hilo linatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa  kiasi cha shilingi milioni 43,954.2; 

(v) Kufanya maboresho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuwezesha  ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa kiwango maalum cha  asimilia tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi wa bomba  la mafuta (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha  gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba husika  kwa kuzingatia masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya  Serikali za Uganda na Tanzania; 

(vi) Kuweka utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji  wadogo wa madini wenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi  milioni 100 kwa mwaka kama ifuatavyo: – 

(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo wa madini kwa kiwango  mfuto cha asilimia 3 kwenye thamani ya mauzo ya madini  pindi yanapopatikana; 

(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi kuwa ni wakati wanapouza  madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini au maeneo maalum yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini; 

(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji mdogo wa madini kama  mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka kwa  wafanyakazi wake pale tu madini yatakapokuwa  yamepatikana na kuuzwa katika masoko ya madini; 

(d) Kuweka muda maalum wa kulipa kodi ya zuio ya ajira  kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini na  kulipa mrabaha katika masoko ya madini au vituo vingine  vya uuzaji na ununuzi wa madini vinayotambuliwa na  Tume ya Madini.

(e) Kuweka kiwango cha kodi cha mapato ya ajira (PAYE) cha  asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini ambayo  italipwa na mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa  niaba ya wafanyakazi wake. 

Amesema kuwa Lengo la mapendekezo hayo ni kurahisisha utozaji na ulipaji wa kodi  kutoka kwa wachimbaji wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza  mchango wa kodi ya mapato kutoka kwenye sekta hiyo. Hatua hizi  kwa pamoja zinatarajia kuongeza mapato ya Serikali shillingi 

milioni 29,776.14 

Kwa upande wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, amesema kuwa Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha  Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya  ushuru wa bidhaa (specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za  petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuvihuisha na mfumuko  wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla.

 Hata hivyo, kutokana  na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za kiuchumi  zilizosababishwa na ugonjwa wa Covid-19, amependekeza  kutofanya mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa  bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli isipokuwa vinywaji  vikali na bia zitakazotengenezwa kwa kutumia shayiri  iliyozalishwa hapa nchini. 

Amependekeza pia kufanya marekebisho  ya Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa kwa  Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa  kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi  765 kwa lita za sasa hadi shilingi 620 kwa lita.

Lengo la  mapendekezo hayo ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini kwa Kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi  na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje  ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa  heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye 

Uvuvi (HS Code 5607.50.00).

Marekebisho hayo ni  kulinda mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya  bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya  Serikali kwa shilingi milioni 2,644

(iii) Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia  10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3  zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711.  Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki  chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 263.7. 

Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli  kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa  kiasi cha shilingi milioni 2,907.7. 

Kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki ya mwaka 2004 Waziri huyu amesema katika  Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti kilichofanyika  tarehe 7 Mei 2021 mjini Arusha, walipendekeza kufanya marekebisho  ya Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha na Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kwa mwaka  wa fedha 2021/22.

Amesema kuwa Mapendekezo hayo yanalenga katika Kuboresha  Maisha ya Watu Kupitia Maendeleo ya Viwanda na Kutengeneza  Ajira kwa ajili ya Ustawi wa Pamoja wa Watu wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki.

Amesema kuwa mapendekezo ya Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa  Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo  zimekuwa zikitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/21.

 Hatua  hizo ni kama Mapendekezo ya hatua mpya za Viwango vya Ushuru wa  Forodha ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mabasi ya abiria  yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99  yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mwendokasi.  Hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa  mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi; 

(b) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba  (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06  na 52.07. Lengo la hatua ni kulinda viwanda  vinavyozalisha bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao la  pamba (value addition) nchini; 

(c) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye matairi mapya ya  pikipiki (new pneumatic tyres of rubber) yanayotambulika  kwa HS Code 4011.40.00. Lengo la hatua ni kuongea  mapato ya Serikali kwa kuwa matairi haya ni bidhaa  zilizokamilika kwa ajili ya mtumiaji; 

(d) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye siagi ya karanga (peanut butter) inayotambulika kwa HS Code 2008.11.00.  Lengo la hatua ni kulinda wazalishaji wa bidhaa hiyo  nchini;

(e) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye nyaya (wire of other  alloy steel) zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na  7229.90.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa 

Kuhusu wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi ni Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye milk cans zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya  maziwa nchini; 

(g) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA (Organic  surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS  Code 3402.11.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo  la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za  unga na maji nchini; 

(h) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10  hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Code 3208.20.00  na 3210.00.10 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa ngozi  nchini; 

(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Codes  2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa  duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  wazalishaji wa mbolea nchini; 

(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  tumbaku iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Code  5310.10.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa tumbaku  nchini; 

(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya chai  iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Codes 4819.20.90,  5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa duty  remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  wachakataji wa chai (tea blenders) nchini; 

(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi ya  kutengeneza masufuria ya aluminium inayotambulika kwa  HS Code 7606.92.00 kwa utaratibu wa duty remission.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa  masufuria hayo nchini; 

(m) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa  pikipiki za matairi matatu bila kujumuisha fremu kwa kuwa  zinatengenezwa hapa nchini (CKD for three-wheel  motorcycles excluding chassis and its components)  zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu  wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili kurahisisha  usafirishaji wa mizigo; 

(n) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au 10  hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za  kutengeneza mabomba ya plastiki (glass reinforced plastic  pipes) zinazotambulika kwa HS Codes 3920.61.10,  7019.39.00, 7019.31.00, 6006.90.00, 7019.12.00, 

3920.10.10, 4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty remission.

Amesema kuwa Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa  watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili kupunguza  gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi wa  miundombinu ya maji; na 

(o) Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka  asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye mabati (Flat-rolled  products of other alloy steel, of a width of 600mm or  more, not further worked than hot-rolled, in coils)  yanayotambulika kwa HS Code 7225.30.00. Lengo la hatua  hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia  bidhaa hiyo kama malighafi. 

(ii) Mapendekezo ya kuendelea na utekelezaji wa Viwango vya  Ushuru wa Forodha vya mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo: 

(a) Kupunguza Ushuru wa Forodha hadi asilimia 0 kutoka  viwango vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25 kwa  mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika  uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika  kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu  (UVIKO-19) vikiwemo Barakoa (Masks), kipukusi 

(sanitizer), mashine za kusaidia kupumua (ventilators),  na mavazi maalum ya kujikinga yanayotumiwa na  madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “duty remission”. Hatua hii  inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa vifaa hivyo hapa  nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa  huo; 

(b) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za  kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali  (Cash registers, Electronic Fiscal Device (EFD) Machines and Point of Sale (POS) machines zinazotambulika katika  HS Code 8470.50.00 na 8470.90.00. Lengo la hatua hii ni  kuhamasisha matumizi ya vifaa hivi katika kuhasibu  mapato ya Serikali; 

(c) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio  vinavyotumiwa na wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu  yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS codes 4819.50.00. Lengo la  hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa  hapa nchini. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika  kutoa unafuu huo; 

(d) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka kiwango cha  asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye  vifuniko vya chupa za mvinyo (corks and stoppers)  vinavyotambulika kwa HS Codes 4503.10.00 kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa nchini. Hatua hii  inalenga kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mvinyo ili  kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la zabibu  nchini pamoja na ajira. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu huo; 

(e) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za  marumaru zinazotambulika kwa HS Code 6907.21.00; 6907.22.00; na 6907.23.00 zinazoingizwa kutoka nje.  Lengo la hatua hii ni kulinda na kukuza viwanda vya  ndani vinavyozalisha marumaru pamoja na kuongeza  ajira;  

(f) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai inayotambulika kwa HS Code 09.02 inayoagizwa kutoka nje. Lengo la pendekezo hilo ni kulinda viwanda vya ndani  na kuhamasisha kilimo cha chai hapa nchini pamoja na  kuongeza ajira katika sekta ya kilimo; 

(g) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia ya kitani (sacks and bags of jute or other textile bast fibers of  heading 53.03) yanayotambulika kwa HS Code  6305.10.00 yanayoagizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii  ni kulinda viwanda vya ndani vinavyotengeneza magunia ya katani, kukuza na kuendeleza kilimo cha zao la  mkonge hapa nchini pamoja na kuongeza ajira na  mapato ya Serikali; 

(h) Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye unga wa kakao  unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code  1805.00.00. Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo  cha zao la kakao nchini pamoja na kuongeza mapato ya  Serikali; 

(i) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya  kusaga kahawa nchini. Vifungashio vitakavyohusika ni vile  vinavyotambulika katika HS codes 7310.21.00;  6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90 na 3920.30.90.  Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la  kahawa na kuvipa unafuu wa gharama viwanda  vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa “Duty  Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo; 

(j) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia korosho. Vifungashio vitakavyohusika ni vile 

vinavyotambulika katika HS code 3923.21.00. Hatua hii  inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho na  kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata  korosho hapa nchini. Aidha utaratibu wa “Duty  Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo; 

(k) Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi  asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya  kuhifadhia pamba. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS codes 3920.30.90;  6305.39.00 na 7217.90.00. Hatua hii inalenga kuvutia  uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la pamba nchini; 

(l) Kupunguza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia  0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye malighafi za kutengeneza taulo za  watoto (Baby Diapers) zinazotumbulika kwa HS code  3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE film HS Code  3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code  6305.33.00, Plastic cask HS Code 3926.90.90; na  kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye Super  Absorbent Polymer HS Code 3906.90.00, Wet strength  paper HS Code 4803.00.00, Non-woven HS Code  5603.11.00, Polyethylene laminated Nonwovens HS Code  5903.90.00, Spandex HS Code 5402.44.00 na Dust free  paper HS Code 4803.00.00. Aidha, msamaha huu  utatolewa kwa utaratibu wa “Duty Remission”. Hatua hii  inatarajiwa kutoa unafuu wa gharama za uzalishaji na kuongeza ajira;  

(m) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye vifaa vinavyotumika katika kukata,  kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito  vinavyotambulika kwa HS Codes 6804.10.00; 7018.90.00; 

7020.00.99; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye  HS Codes 3606.90.00; 6813.20.00; 8202.20.00;  8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90;  8513.10.90; na 9002.19.00. Hatua hii inalenga kuchochea  uongezaji wa thamani kwenye madini. Utaratibu wa  “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifaa hivyo;  

(n) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye makaratasi (HS Code 4805.24.00 na  4805.25.00) yanayotumika kama malighafi ya  kutengeneza vifungashio aina ya maboksi (corrugated  boxes). Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika. Lengo  la hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa vifungashio  hivyo hapa nchini ili wananchi waweze kuvipata kwa bei  nafuu; 

(o) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwenye vifungashio vya mbegu  vinavyotambulika katika HS codes 3923.29.00;  6305.10.00; 4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00;  6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90. Utaratibu  utakaotumika kutoa unafuu huo ni wa “duty remission”.  Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa  mbegu hapa nchini; 

(p) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye kahawa  inayotambulika kwa Heading 09.01 inayoagizwa kutoka  nje ya nchi. Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda  vya ndani na kuhamasisha kilimo cha kahawa hapa nchini 

pamoja na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo;  

(q) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za  kimarekani 125 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea  kiwango kitakachokuwa kikubwa. Bidhaa hizo ni “Flat – rolled products of iron or Non-alloy steel na Flat –rolled  products of other alloy steel.” Bidhaa hizi hutambulika  katika HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00;  7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00; 

7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0 na 7226.92.00.  Lengo la kuendelea kutoza viwango hivyo ni kulinda  viwanda vya hapa nchini, kukuza ajira pamoja na  kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo  kutoka nje; 

(r) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS codes  7210.41.00; 7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00;  7210.70.00 na 7210.90.00 kutegemea kiwango  kitakachokuwa kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25  au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo 

(metric ton), kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni  kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini  kutokana na ushindani wa nje; 

(s) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika katika  HS Code 7212.60.00 badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani  kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa  hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;

(t) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Ushuru huo unahusu  bidhaa zinazotambulika katika HS Code 7212.30.00;  7212.40.00 na 7212.50,00. Hatua hii ina lengo la kulinda  viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani  halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under invoicing and under valuation), na kulinda ajira na  mapato ya Serikali; 

(u) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za  kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au  dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo  (metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja  kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye  nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow  profile). Hatua hii inahusu bidhaa zinazotambulika katika  HS codes 7213.10.00; 7213.20.00; 7213.99.00;  7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00; 7214.90.00;  7214.99.00; 7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00;  7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00; 7306.30.00;  7306.50.00; 7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00.  Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha  nondo hapa nchini na kuongeza ajira; 

(v) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya  asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mboga  mboga (horticultural products) zinazotambulika kwa HS  codes 0603.11.00; 0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00;  0603.15.00; 0603.19.00; 0604.20.00; 0604.90.00;  0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00; 0703.20.00;  0703.90.00; 0706.10.00; 0706.90.00; 0710.10.00;  0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00; 0714.10.00;  0714.20.00; 0804.30.00; 0804.40.00; 0804.50.00; 

0805.10.00; 0805.40.00; 0805.50.00; 0806.10.00;  0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00; 0808.30.00;  0910.11.00 na 0910.12.00. Lengo la hatua hii ni kulinda  wakulima wa ndani ili kuendeleza kilimo cha matunda,  mbogamboga na maua hapa nchini;  

(w) Kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 10  badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa  za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code  3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika  kwa ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha  n.k. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali; 

(x) Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya  asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi  zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo  zinazotambulika kwa HS codes 4804.11.00; 4804.21.00;  4804.29.00; 4804.31.00 na 4804.41.00. Lengo la hatua  hii ni kuendelea kulinda viwanda vinavyozalisha karatasi  hizo hapa nchini; 

(y) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code  1001.99.10 na HS Code 1001.99.90 kwa utaratibu wa  “Duty Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu  ni wenye viwanda vya kusaga ngano. Lengo la hatua hii  ni kupunguza gharama kwa Viwanda vinavyozalisha unga  wa ngano; 

(z) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 25 kwa utaratibu wa duty remission kwenye  bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier  Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90 ambayo hutumika 

kama malighafi ya kutengeneza vifungashio vya dawa ya  meno kwenye viwanda vya ndani. Lengo la hatua hii ni  kutoa unafuu wa gharama kwa viwanda vinavyozalisha  dawa ya meno nchini; 

(aa) Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0  kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha  asilimia 10 kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye  malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD  Palm Stearin (HS Code 1511.90.40) kwa viwanda 

vinavyotengeneza sabuni nchini. Lengo la hatua hii ni  kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni nchini; 

(bb) Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa  asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa kilo moja ya  viberiti (safety match boxes) vinavyotambuliwa kwenye  HS code 3605.00.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa  kikubwa badala ya asilimia 25 pekee. Lengo la hatua hii  ni kulinda viwanda vinavyozalisha viberiti nchini dhidi ya  bidhaa zenye ruzuku kutoka nje na hivyo kuwa na  ushindani sawa katika soko.

odi ya Nyama Tanzania

Kutoza ada ya shilingi 70,000 kwa Cheti cha Kukubaliwa kupeleka nyama nje ya Nchi badala ya kiwango cha asilimia 1 ya malipwani.


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)

Kupunguza tozo ya ukaguzi wa Umeme kwa kipimo kimoja (electrical inspection, electrical insulation test and general inspection) kutoka shilingi 590,000 hadi 150,000. Tozo hii inatozwa kabla ya kuanza biashara ya mafuta. Pendekezo hili linatarajia kuchochea mazingira wezeshi ya biashara nchini hususan katika maeneo ya vijijini.




Utoaji Leseni za Bima kwa Makampuni

Napendekeza kubadili utaratibu wa sasa wa makampuni ya bima kulazimika kuomba leseni upya kila mwaka na badala yake makampuni yanayofanya vizuri yawe na leseni ya kudumu, na makampuni yalioko kwenye hali ya uangalizi yapewe leseni ya miaka mitatu huku yakiwa kwenye uangalizi na yakiimarika na kufanya vizuri yaingie kwenye leseni za kudumu. Taratibu za ufuatiliaji na malipo ya kila mwaka yaendelee kama ilivyo sasa. Lengo ni kupunguza ukiritimba.

Uboreshaji wa Mazingira ya Ufanyaji Biashara

Sambamba na hatua za kikodi zilizolenga kupunguza gharama ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara, Serikali itakamilisha mfumo wa kimtandao wa kuwa na dirisha moja la upatikanaji wa vibali mbalimbali katika Idara zote zinazohusika na usajili na vibali ili kuwapunguzia wawekezaji mizunguko ya kutembea ofisi zaidi ya moja kuhangaika nenda rudi kutafuta vibali vinavyotolewana ofisi zaidi ya moja. Lengo la hatua hii nikurahisisha mazingira ya kufanya biashara kama ilivyobainishwa kwenye Blueprint.

Maeneo Mahususi

Barabara za Mijini na Vijijini

Mheshimiwa Spika, hali ya barabara vijijini hairidhishi ambapo bado vipo vijiji ambavyo havina barabara kabisa. Barabara nyingi zinazosimamiwa na TARURA zina hali mbaya. Kwa sasa mtandao wa barabara zilizo chini ya TARURA una urefu usiopungua kilomita 108,946.2 ambazo zinaunganisha maeneo mbalimbali ya mijini na vijijini. Hadi Desemba 2020, mtandao wa barabara zilizo chini ya TARURA wenye kiwango cha lami ulifikia kilometa 2,250.69, sawa na asilimia 2.1 tu, changarawe kilometa 27,809.26 (asilimia 25.6) na udongo kilometa 78,886.25 (asilimia 72.4).

Mheshimiwa Spika, hali hii ya barabara ina madhara makubwa sana kwa jamii yetu kwani baadhi ya akina mama wajawazito wanapoteza maisha kwa kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya. Aidha, wapo wengine ambao wanajifungulia njiani kutokana na kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya. Vilevile, wapo baadhi ya wanafunzi wanaosombwa na maji na kufariki kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, hususan katika maeneo ya vijijini. Kadhalika, bado kuna changamoto ya usafirishaji wa mazao na bidhaa kutoka au kwenda barabara kuu katika baadhi ya maeneo. Serikali imeona ipo haja ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuongezea katika mgawo wa sasa kupitia Mfuko wa Barabara ili kufanikisha ugharamiaji wa mtandao wa barabara hizo.




Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Mijini na Vijijini

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa maji safi na salama mijini na vijijini bado hairidhishi. Maji hayana mbadala, maji ni uhai, maji ni maisha kwa viumbe hai vyote. Bado vipo vijiji ambavyo havina kisima hata kimoja cha maji safi na salama na badala yake hutumia maji ya mapalio, maji ya madimbwi, maji ya mito wanayochangia na wanyama. Tanzania ina vyanzo vikubwa na vya uhakika vya maji ikiwa ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, Ziwa Chala, Mto Kiwira, Ruvu, Rufiji na Ruvuma pamoja na mingine. Aidha, kuna uwezekano wa kutumia mabwawa makubwa kama ya Kidunda, Ndembela na Farkwa kama yangekamilika lakini utekelezaji wake haujaanza pamoja na fidia kutolewa na Serikali kutokana na uhaba wa fedha. Ipo miradi mingi katika mikoa ya Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora, Tanga na Simiyu inayotakiwa kutekelezwa katika mwaka 2021/22, lakini haikuwa katika bajeti. Mikoa mingine ambayo sikuitaja hapa iko kwenye bajeti ya Wizara husika.




Mheshimiwa Spika, hali ya ukosefu wa maji safi na salama ina madhara makubwa sana kwa jamii yetu. Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa inampa nafuu mwanamke katika kufanya shughuli zake za kiuchumi, lengo likiwa ni kumtua mama ndoo kichwani na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakumba akina mama na mabinti katika harakati za kutafuta maji. Aidha, kuna baadhi ya wanafunzi wanakosa masomo na kuharibu maisha yao kutokana na uhaba wa maji katika maeneo yao. Hivyo, Serikali imeona ipo haja ya kuongeza fedha za kugharamia miradi ya maji kwa kubuni vyanzo mbadala vya mapato kwa ajili ya kugharamia miradi ya maji hususan katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji.

Afya na Bima ya Afya kwa Wote

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Afya ni sekta muhimu katika ustawi wa jamii yetu na ni moja ya mahitaji muhimu sana katika maisha ya sasa ya mwanadamu. Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana katika sekta hii, ingawa bado kuna kazi kubwa ya kufanya kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na mabadiliko ya hali za kiafya kwenye kizazi cha leo. Aidha, wananchi katika maeneo mbalimbali wametumia nguvu kubwa katika kutafuta ufumbuzi wa masuala ya upatikanaji wa huduma za afya kwa kujenga maboma karibu na maeneo yao. 
 
Majengo yaliojengwa kwa nguvu za wananchi yamekaa kwa muda mrefu, kati ya miaka mitano (5) hadi 15. Hadi kufikia Juni 2021, kuna jumla ya maboma 8,004 ya zahanati ambayo yapo katika mikoa mbalimbali nchini na yapo katika hatua mbalimbali za kukamilishwa. Vilevile, yapo maboma kwenye ngazi ya vituo vya afya zaidi ya 1,500 ambayo yametumia nguvu ya wananchi na yanahitaji kukamilishwa. Serikali itaendelea na jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma hayo pamoja na kuajiri wataalamu wa afya na kuimarisha upatikanaji wa dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba.

Mheshimiwa Spika, kuna mradi mkubwa wa bima kwa wote (Universal Health Care) unaolenga kuwafikia watanzania wote. Tanzania ina jumla ya kaya milioni 12.827, ambapo asilimia 20 ya kaya hizo inakadiriwa kuwa ni kaya zisizokuwa na uwezo. Katika kufanikisha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya kwa wananchi wote, Serikali itahitaji zaidi ya shilingi bilioni 149 katika mwaka wa kwanza kwa ajili ya kaya zisizo na uwezo. Kiasi hicho cha fedha kitaendelea kuongezwa kila mwaka ili ifikapo mwaka 2034/35, wananchi wote wawe wamefikiwa na bima ya afya. Serikali imeendelea kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambapo vituo vya kutolea huduma za afya kwa ngazi mbalimbali vimeendelea kujengwa ili bima ya Afya iweze kutumika na kuwanufaisha wananchi wote.

Elimu

Mheshimiwa Spika, kuhusu sekta ya elimu kuna kazi kubwa bado iko mbele yetu. Bado kuna shule ambazo zina wanafunzi wengi kuliko idadi ya madarasa na zipo zinazogawa mikondo ili wanafunzi wengine wasome asubuhi na wengine wasome mchana. Hali hii inapunguza muda wa wanafunzi kusoma. Zipo shule ambazo kwenye darasa moja wanaweka uzio wa ubao kutenganisha ili chumba kimoja wasome wanafunzi wa madaraja mawili. Aidha, zipo shule ambazo miundombinu yake imechakaa sana kiasi cha kutishia usalama wa watoto na walimu wetu. Yapo pia madarasa yaliyoezekwa kwa nyasi na yana sakafu ya vumbi. Kadhalika, mwaka ujao utakuwa wa kwanza wa kupokea wanafunzi kidato cha kwanza waliodahiliwa darasa la kwanza kwa mpango wa elimumsingi bila ada. Jambo hili lisipoangaliwa mapema litakuja kusababisha wanafunzi kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na kukosa pa kwenda hadi miundombinu ijengwe kwa zimamoto. Kwa hatua ya maendeleo nchi yetu iliyofikia katika sekta mbalimbali, hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Kujenga miundombinu ya shule zetu kwa kusubiri irushwe kwenye mitandao ya kijamii ndio tuone inatutia aibu, au kusubiri watoto wakose pa kwenda au wakose pa kukaa ndipo tukimbizane na kufukuzana, ni ishara ya kutopanga vizuri. Hili tusingependa liendelee kuwepo.

Mheshimiwa Spika, kila mwaka kuna wanafunzi kati ya asilimia 15 - 20 wanatoka kwenye mfumo wa elimu kwa kutoendelea na kidato cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kupata ujauzito, utoro na hali ngumu ya maisha. Ukosefu wa mpango wa kugharamia mahitaji ya sekta ya elimu ndiyo chanzo cha tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa elimu ya juu, zaidi ya wanafunzi 11,000 wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu ambao tayari walishapata udahili katika vyuo mbalimbali walikosa mikopo. Naongelea mkopo, sio fedha ya bure, bali ni mkopo ambao ataurejesha. Katika jamii nyingi za kitanzania, mtoto akikosa mkopo huku akiwaona wenzake wanaendelea, inamfadhaisha sana. Ni mfadhaiko kwake na familia nzima. Kwa hatua ya maendeleo ambayo nchi yetu imepata katika sekta mbalimbali hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Serikali inakusudia kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa inaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwanufaisha vijana wote wenye sifa za kupata mkopo.

Miradi ya Kielelezo ya Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Nyerere na Reli ya Kisasa (SGR)

Mheshimiwa Spika, Miradi ya bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na Reli ya Kisasa (SGR) sio tu ni miradi ya kielelezo bali ni miradi mama kwa kila mtanzania. Ni miradi inayoashiria uhuru wa nchi yetu, ni miradi inayoashiria kujitegemea kwa nchi yetu, ni miradi inayoashiria heshima ya mtanzania na inajengwa na mtanzania. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais, kutokamilika kwa miradi hii itakuwa laana kwa Taifa letu. Hatutajengewa miradi hii na mtu yeyote, tutawaenzi wabeba maono wa miradi hii kwa kujenga na kuikamilisha. Mwalimu Nyerere alibeba maono ya miradi hii, Rais Magufuli alianzisha miradi hii, Rais Samia anakwenda kuijenga miradi hii. Niwahakikishie watanzania hapatakuwepo GOFU hata la Mradi mmoja wala kusimama kwa mradi unaotekelezwa hata kwa mwezi mmoja.


Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na maeneo mahsusi hayo niliyotangulia kuyasema, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria zifuatazo:

Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, SURA 220

Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta kama ifuatavyo:

Kuongeza Ushuru wa barabara kwa shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli;

Kufanya marekebisho ya kifungu cha 4 A(a) cha sheria ili kuelekeza fedha zitakazokusanywa kutokana na ongezeko la ushuru wa barabara na mafuta la shilingi 100 kwa aina zote za mafuta ziwe kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara za vijijini kupitia TARURA.

Hatua hii ya marekebisho ya Sheria inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 322,158.20.

Sheria ya Petroli, SURA 392

Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Petroli ili kuongeza tozo ya Mafuta ya Taa kutoka shillingi 150 hadi shillingi 250. Lengo la hatua hii ni kupunguza uchakachuaji wa mafuta kufuatia ongezeko la ushuru wa mafuta kwenye dizeli na petroli.

Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306

Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki kama ifuatavyo:

Kutoza tozo ya shillingi 10 hadi shilingi 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14; na

Kutoza kiasi cha shilingi 10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 396,306.0.

Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147

Kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango kikubwa cha kilevi, napendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii inatarajia kuiongezea mapato Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 60,769.35.

Utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,033,639.66.

Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi.

Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo. Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).

Njia Mbadala za Kutekeleza Miradi Mikubwa

Mheshimiwa Spika, mwaka 2020 nchi yetu ilifanikiwa kuingia katika kundi la nchi zenye kipato cha kati cha chini (Lower Middle-Income Country). Kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati kunaifanya nchi yetu kutakiwa kujiendesha kiuchumi bila kutegemea kwa kiwango kikubwa misaada na mikopo yenye masharti nafuu ambayo, hupewa nchi zenye kipato cha chini. Hivyo, ni lazima Serikali iboreshe mbinu inazotumia na kubuni mbinu mpya za kupata mapato. Katika kutekeleza hatua hii, Serikali imeanza kufanya uchambuzi wa vyanzo mbadala vya rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama vile ufadhili mchanganyiko (Blended Finance). Wafadhili wanaotoa aina hii ya ufadhili hutoa fursa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania, kurekebisha au kujumuisha (restructuring or consolidation) deni lake kwa makubaliano ya kutumia sehemu ya malipo ya deni katika uhifadhi wa mazingira au kuimarisha sekta za kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2021/22, Serikali inadhamiria kukamilisha mchakato wa Tathmini na Ukadiriaji wa Kukopesheka kwa Nchi (Sovereign Credit Rating). Hatua hii inalenga kutuwezesha kujua nafasi yetu katika masoko ya fedha ya kimataifa na jinsi wakopeshaji wanavyotuona hasa katika uwezo wa kusimamia uchumi na kulipa madeni yetu. Hatua hiyo itatuwezesha pia kuongeza wigo wa wakopeshaji ambao wako tayari kutukopesha, hususan katika Masoko ya Mitaji ya Kimataifa (International Capital Markets). Serikali itaanza mara moja mchakato wa wazi wa kutekeleza na kukamilisha kazi ya Sovereign Credit Rating ndani ya mwaka 2021/22.

Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kupanua wigo wa vyanzo vya rasilimali fedha, Serikali itaangalia uwezekano wa kutumia Hati Fungani zitakazotolewa na Halmashauri za Manispaa na Majiji kama njia mbadala ya kupata rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Hatua hii itapunguza mzigo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali hasa kwa Halmashauri zenye miradi ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu na kuwa na uhakika wa uwezo wa miradi hii kujiendesha kwa faida (bankable projects). Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (United National Capital Development Fund - UNCDF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (Capital Markets and Securities Authority - CMSA) imeanza mchakato wa kuhakikisha kwamba Halmashauri, Manispaa na Majiji yatakayokidhi vigezo na masharti ya matumizi ya Hati Fungani hizi yanaanza kutumia utaratibu huu.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaona umuhimu wa kutumia Masoko ya Hati Fungani za Kimataifa maarufu kama Eurobonds ikiwa ni chanzo cha kuaminika na thabiti cha kugharamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia Mkakati wa Deni la Muda wa Kati (Medium Term Debt Strategy - MTDS). Hatua hii inakwenda sambamba na hatua nyingine inayopendekezwa katika hotuba hii ya kufungua soko la dhamana za Serikali ili kuruhusu wawekezaji wa nje ya Tanzania na Afrika Mashariki kununua hati fungani zetu ili kuongeza ukwasi katika soko la ndani.

Mheshimiwa Spika, Soko la Eurobond ulimwenguni linakadiriwa kuwa na zaidi ya dola za Marekani trilioni 30 zilizotolewa kwa nchi zinazotafuta rasilimali fedha kwa njia ya mikopo kutoka kwenye masoko ya kimataifa yenye ukwasi mkubwa ili kugharamia miradi ya maendeleo. Njia hii pia hutumiwa na mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika wanapotafuta fedha kwa ajili ya kufadhili miradi yao kote duniani. Aidha, nchi mbalimbali za kusini mwa Jangwa la Sahara zinazofanya vizuri kiuchumi zimekuwa zikitumia Soko la eurobond kama chanzo thabiti na chenye masharti rafiki katika kugharamia utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo. Tanzania itahitaji kufanyiwa tathmini ya kukopesheka ili kufikia masoko ya mitaji ya kimataifa kupitia eurobonds. Hivyo, zoezi la kukadiria au kutathmini kukopesheka kwa Tanzania ni hatua isiyoepukika.

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2010 tulipopitisha Sheria ya PPP hatujapata mafanikio ya kujivunia katika eneo hili pamoja na faida kubwa na nyingi ambazo Taifa linaweza kupata kupitia mfumo wa PPP hasa katika miradi mikubwa inayohitaji fedha nyingi na utaalamu kutoka sekta binafsi. Utekelezaji wa miradi ya PPP hupunguza mzigo kwenye deni la Serikali na hata katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na hutoa nafuu ya kibajeti (Fiscal Space) kwa kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu mengine ambayo hayawezi kugharamiwa na sekta binafsi. Hivyo, ni muhimu kutumia PPP kwenye miradi mbalimbali inayokidhi Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura 103.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia manufaa ya PPP, Serikali itaongeza kasi ya kushughulikia miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ikiwa ni pamoja na: Ujenzi wa viwanda vya dawa muhimu na vifaa tiba; ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo Changamani cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara; na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Aidha, wananchi na wawekezaji wengine wanaalikwa kubainisha maeneo ambayo wanaweza kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya PPP kulingana na uwezo wao wa mitaji na utaalamu.

SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2021/22

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia shabaha, malengo pamoja na sera za bajeti kwa mwaka 2021/22, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 36.33 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika. Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 26.03, sawa na asilimia 71.7 ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 22.18, sawa na asilimia 13.5 ya Pato la Taifa. Aidha, Serikali inalenga kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya shilingi trilioni 2.99 na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri shilingi bilioni 863.9.

Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo wanatarajia kuchangia misaada na mikopo nafuu yenye jumla ya shilingi trilioni 2.96, sawa na asilimia 8.1 ya bajeti yote. Kiasi hicho kinajumuisha fedha za miradi ya maendeleo shilingi trilioni 2.67 na Mifuko ya Pamoja ya Kisekta shilingi bilioni 282.3. Napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kutoa fedha za misaada na mikopo nafuu ili kufanikisha miradi na programu mbalimbali za maendeleo zitakazotekelezwa katika bajeti ya mwaka 2021/22.

Mheshimiwa Spika, kipekee ningependa kuwatambua Washirika wetu wa Maendeleo kama ifuatavyo: Serikali za Canada, China, Denmark, Finland, India, Ireland, Italia, Korea ya Kusini, Japan,Ufaransa, Ujerumani, Norway, Poland, Ubelgiji, Uholanzi, Uswisi, Uingereza, Sweden na Marekani. Vilevile, kuna Mashirika ya Kimataifa ambayo ni Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi katika Afrika, Mfuko wa Abu Dhabi, Mfuko wa Kuwait, Mfuko wa kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi, kifua kikuu na malaria, Umoja wa Ulaya, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Umoja wa mataifa na mashirika yote yaliyopo chini yake, Mfuko wa OPEC kwa Maendeleo ya Kimataifa, Mfuko wa Mazingira, pamoja na Shirikisho la GAVI. Ninapenda pia kuyatambua Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya ndani na nje pamoja na mashirika ya ufadhili - philanthropies kwa misaada yao kwenye sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 7.34 kutoka soko la ndani na nje kwa masharti ya kibiashara. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 4.99 ni mikopo ya ndani ambayo inajumuisha shilingi trilioni 3.15 kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na shilingi trilioni 1.84 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Aidha, shilingi trilioni 2.35 zinatarajiwa kukopwa kutoka soko la nje kwa lengo la kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2021/22, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 36.33 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 23.0 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 13.33 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zinajumuisha shilingi trilioni 10.66 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali, shilingi trilioni 8.15 kwa ajili ya mishahara na shilingi trilioni 4.19 kwa ajili ya matumizi mengineyo. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 200.0 kwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya watumishi, wazabuni na watoa huduma.

Mheshimiwa Spika, jumla ya shilingi trilioni 13.33 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, sawa na asilimia 37 ya bajeti yote. Kati ya kiasi hicho, fedha za ndani ni shilingi trilioni 10.37 na fedha za nje shilingi trilioni 2.96. Aidha, fedha za maendeleo zinajumuisha, shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya miradi ya reli ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa; shilingi trilioni 2.08 kwa ajili ya miradi ya barabara, ujenzi wa madaraja, na viwanja vya ndege; shilingi trilioni 2.34 kwa ajili ya miradi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere; shilingi bilioni 589.4 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini; shilingi bilioni 233.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi; shilingi bilioni 500 ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu; shilingi bilioni 215.6 kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022; na shilingi bilioni 312.1 kwa ajili ya elimumsingi bila ada. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 400.0 kwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya miradi ya maendeleo.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, ninapoelekea mwisho wa hotuba hii, napenda kumshukuru kwa dhati MAMA YETU kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Ninamuahidi Mheshimiwa Rais, Waheshimiwa wabunge na Watanzania wote kwamba, nitaibeba dhamana hii kwa uadilifu, weledi na uwezo wangu wote na ninamuomba Mwenyezi Mungu anijalie afya njema, hekima na busara katika kutekeleza majukumu hayo. Naomba nielezee masuala machache muhimu kabla ya kuhitimisha hotuba hii.

Mheshimiwa Spika, kwanza natoa pongezi kwa MAMA YETU kwa matumaini makubwa aliyowapa watanzania. MAMA YETU ameonesha ni Kiongozi Makini, ni Kiongozi Shupavu, ni Kiongozi Mchapa Kazi, ni Kiongozi Mwadilifu, ni Kiongozi Msikivu, ni Kiongozi aliye na dira thabiti na maono ya kuendelea kuiletea nchi yetu maendeleo makubwa. Ameweka wazi kuwa hataki kodi ya dhuluma, hataki kuendesha Serikali kwa mapato ya dhuluma, ameweka wazi kusimama imara kwenye masuala ya mapato na matumizi ya Serikali, ameweka wazi kuwa atakuwa imara kwenye vita dhidi ya rushwa.

Mheshimiwa Spika, kwa kauli hizo MAMA YETU ameonesha kuwa, kukaa kwake katika nafasi mbalimbali katika Serikali za awamu mbalimbali SMT na SMZ kumemfanya awe kiongozi aliyeandaliwa na KUIVA na aliye tayari kuiongoza nchi kwa ufanisi mkubwa. Itakumbukwa mbali na nafasi zingine nyingi alizoshika katika miaka yake takribani ishirini Serikalini, MAMA YETU amekuwa Waziri katika Awamu ya Nne na amekuwa Makamu wa Rais katika Awamu ya Tano. Kuna style za uongozi amejifunza.

Mheshimiwa Spika kuna style za uongozi amejifunza kupitia Awamu hizo alikopewa nafasi kuhudumu katika nafasi mbalimbali. MAMA YETU alikuwa Waziri katika awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mheshimiwa Kikwete alikuwa Mzalendo wa kweli, alikuwa na maono (Visionary Leader), alikuwa mwalimu, alikuwa mzazi, alikuwa mlezi na kiongozi, alikuwa rahim sana, alikuwa mvumilivu sana aliyeamini kwenye Mifumo, Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi. Hii naweza kuifananisha kama Refa kwenye mchezo wa mpira wa miguu, ambaye anachezesha mechi zake akiwa na kadi ya njano tu, kadi nyekundu anaiacha nyumbani. Ukicheza rafu mara ya kwanza anakuonya kwa kukuelekeza, ukicheza rafu mara ya pili anakupa kadi ya njano, ukikosea anakupa kadi ya njano tena na alipotakiwa kutoa kadi nyekundu mara nyingi alionya kwa mdomo, kwa kuwa kadi nyekundu alikuwa anaiacha nyumbani. Rais Kikwete aliamini sana kwenye Mifumo na Utendaji wa Kitaasisi. Kwa mtazamo wangu, jinsi MAMA YETU alivyoanza ni dhahiri amepata funzo kwenye awamu hiyo ikiwemo funzo la Uzalendo, maono na kuamini kwenye Mifumo, Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi”, na hapa naweza kusema ameichukua kadi ya njano, anayo na ameanza kutumia kama mnavyoona.

Mheshimiwa Spika, MAMA YETU alikuwa Makamu wa Rais katika awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli, alikuwa na Maono (Visionary Leader), alijitoa kwa nguvu zote (Dedicated), alikuwa na uthubutu sana, mtu wa vitendo sana na muumini wa matokeo na kuchukua hatua za papo kwa papo. Kama refa wa mchezo wa mpira wa miguu, alikuwa akienda kuchezesha Mechi zake akiwa na kadi nyekundu tu, kadi ya njano alikuwa anaiacha nyumbani. Ukicheza rafu mara ya kwanza tu anakupa kadi nyekundu, wakati mwingine hata asipoiona rafu yeye, mchezaji au shabiki akisema ameona rafu anakupa kadi Nyekundu (no nonsense), hata mimi mwenyewe niliwahi kutembelewa na kadi nyekundu nikakosa michezo kadhaa. Hayati Dkt. Magufuli aliamini kwenye nidhamu ya hali ya juu ya mchezo. MAMA YETU alikuwa Line one na Mheshimiwa Majaliwa akiwa Line two. Hivyo, MAMA YETU amepata mafunzo kwenye awamu hiyo ya Uzalendo, Uthubutu, mtu wa vitendo kuamini kwenye matokeo na nidhamu kazini na ameichukua kadi ya nyekundu.

Mheshimiwa Spika kuna style za uongozi amejifunza. MAMA YETU anazo kadi zote, kadi ya njano na kadi nyekundu. MAMA YETU ni Mzalendo wa kweli, ni Mwadilifu sana, ana Uthubutu, ana Maono, anaamini kwenye Mifumo, Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi”, hataki maneno anataka vitendo. Nitoe rai kwa watumishi wote wa umma na watanzania kwa ujumla tuchape kazi kwa bidii, kwa uadilifu na uzalendo mkubwa. Kwa watumishi wa umma tusimamie matumizi ya fedha za walipa kodi kwa uadilifu mkubwa na kwa watanzania tulipe kodi bila shuruti. Tabia moja ya refa asiyependa kuonea upande wowote, huwa hawezi kupendelea upande wowote. Kwenye michezo ya mieleka huwa mnapewa tahadhari ya dont try this at home, kwenye maslahi ya nchi wanaotaka kumjaribu MAMA YETU nawaonya “Dont try at all”. Tujiepushe na kadi Nyekundu.

Mheshimiwa Spika, lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu mali na rasilimali hapa nchini (mali za umma na mali binafsi). Kwa upande wa mali za umma, lazima tutangulize uzalendo na uadilifu tunapotekeleza majukumu yetu. Serikali inapoteza fedha nyingi kwenye kutekeleza Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa kutojali thamani ya fedha kwenye miradi. Watumishi wa Serikali wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuongeza gharama za miradi ikilinganishwa na gharama halisi ingawa wanafuata taratibu zote za ununuzi. Taratibu za ununuzi zinapokamilika, watumishi na wafanyabiashara hawa hugawana fedha na kiasi kidogo tu kilichosalia ndicho kinaelekezwa kwenye mradi husika na hatimaye kupata mradi ulio chini ya kiwango. Ukiwafuatilia kisheria hupati moja kwa moja pa kuwashika, hivyo wanakuwa wameiba kwa kuzingatia sheria. Nawaelekeza wote wanaohusika na ununuzi wa umma kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na kutanguliza mbele uzalendo na uadilifu. Serikali itachukua hatua za makusudi katika kuimarisha usimamizi wa sheria na taratibu za ununuzi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mali binafsi, ni lazima tuheshimu biashara zetu na mali zinazotokana na biashara hizo. Kuna hatua tunazozifanya sekta zote za umma na binafsi zinadumaza uchumi wetu. Kwa mfano, kuna tabia ya kutolipa madeni kwenye benki zetu, jambo ambalo linapunguza uwezo wa benki kutoa mikopo kwa watu wengine. Aidha, wapo watu wengine ambao wakidaiwa kwa makusudi ya kuchelewesha malipo wanakimbilia mahakamani. Tusitumie vibaya vyombo vyetu vya sheria. Vilevile, kuna baadhi ya wakopeshaji ambao hawaheshimu mali za wateja wao. Mfano, mteja anakuwa amelipa sehemu kubwa ya mkopo wake lakini ikitokea mkopeshaji, rafiki au dalali akaipenda dhamana iliyowekwa, hufanya njama ya kupiga mnada dhamana hiyo kwa bei isiyolingana na thamani ya dhamana au sehemu ya deni iliyobaki sio hata robo ya dhamana hiyo. Natoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kila eneo panapokuwa na minada kwenye sekta binafsi na hata sekta ya umma na pale patakapoonekana kuwepo kwa njama za kudhulumu wamiliki wa mali au kuchepusha sehemu ya mali zinazouzwa kwa mnada hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Kuna wanaodhani tunapoongelea kukusanya kwa weledi, sheria na haki wanachukulia tutaacha kukusanya kodi. Nataka nisisitize kuwa, tutakusanya Mapato ya Serikali. Tutakusanya Mapato ya Serikali. Tutakusanya Mapato ya Serikali. Nitoe rai kwa watumishi wote wa Serikali wanaohusika na kukusanya kodi, maduhuli na ushuru kuelewa vizuri maelekezo haya kwa kuzingatia sheria, weledi na kutenda haki kama Mheshimiwa Rais alivyoelekeza. Nimeanza kusikia visingizio kila kona, mara mfumo, mara mtandao mara EFD haifanyi kazi. Kwa watoza kodi na walipakodi wote visingizio hivi vitaturudisha kwenye ukaguzi. Tusiwekeze kwenye kusaidiwa kukwepa kodi bali tusaidiwe kwenye kufuata sheria. Akiwepo mtumishi akakusaidia kukwepa kodi nawe ukampa asante unatengeneza tatizo tu sio unafuu kwani kuna siku utakuja kukaguliwa huku aliyekusaidia akiwa amehamishwa au kuachishwa kazi. Nitumie fursa hii kumwelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato kuweka watu mahususi wa kufanya doria kila kona, nchi nzima kuangalia mwenendo wa matumizi sahihi ya EFD na mifumo mingine ya malipo kuwa muda wote inafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, tutasimamia nidhamu katika matumizi. Tutasimamia nidhamu katika matumizi. Tutasimamia nidhamu katika matumizi na tutaendeleza mapambano dhidi ya Rushwa na Ufisadi. Nazijua mbinu zote za udanganyifu, nazijua njia zote za majizi na watakaoendelea na tabia za kudokoadokoa fedha za walipa kodi, nitawashukia kama mwewe. Kazi inaendelea, watanzania endeleeni kumwamini Mheshimiwa Rais wetu, yuko macho na wasaidizi wake tuko macho, tutapambana na MCHWA wote, kuna mengine mnayasikia, kuna mengine mnayaona na mengine hata hamyaoni, yote tunaendelea kuyafanyia kazi kwa maelekezo thabiti na ya kizalendo ya Mheshimiwa Rais wetu. Kinyiramba kuna msemo usemao MWINDA KANGA HAPIGI YOWE.”

Mheshimiwa Spika, tuendeleze kwa kasi na kukamilisha miradi ya kimkakati ambayo inalenga kukuza uchumi, kuimarisha huduma za jamii na kuongeza fursa za ajira, hususan ajira kwa vijana. Tutakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, tutaendelea na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) mpaka itakamilika, tutamalizia ujenzi wa barabara zinazounganisha mikoa zilizosalia, tutakamilisha ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi na madaraja mengine kuwaunganisha wananchi wetu, tutaendelea na usambazaji wa umeme kutoka kila kijiji kwenda kila kitongoji na hatimaye kila nyumba.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Jiji la Dodoma na kulifanya kuwa la kisasa. Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa ofisi za wizara na taasisi zake katika mji wa Serikali Mtumba; kujenga barabara za mzunguko; na kuboresha miundombinu ya maji. Aidha, Serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais amenituma niwahakikishie watanzania kupitia hotuba hii kuwa, tunaendelea kuijenga nchi, tunaendelea kuijenga nchi, ije mvua, lije jua, tunaendelea kuijenga nchi, uwe usiku au mchana, tunaendelea kuijenga nchi. Hakuna mradi hata mmoja utakaokwama, wala hakuna Sekta ya maendeleo itakayozorota. KAZI INAENDELEA.”

Mheshimiwa Spika, nampongeza Dkt. Philip Isdor Mpango aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na kuthibitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, napenda kumpongeza kwa dhati kwa kazi nzuri aliyoifanya katika usimamizi wa uchumi kama Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano ulioiwezesha nchi yetu kuingia katika kundi la nchi za hadhi ya uchumi wa kipato cha kati cha chini. Vilevile, nampongeza kwa kazi nzuri iliyotukuka katika kuisimamia Wizara ya Fedha na Mipango ambayo kwa hakika imeweka msingi mzuri wa utekelezaji wa majukumu yangu.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe Rais Mwinyi, ameanza kazi vizuri sana na kuwapa matumaini mapya wananchi wa Zanzibar katika kukuza uchumi na maendeleo hasa kwa kuwekeza kwenye Blue Economy”.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kwa kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nampongeza kwa uongozi wake hodari ndani ya Serikali na hapa Bungeni pamoja na kuendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.

Mheshimiwa Spika, naomba niwapongeze wakuu wa mihimili mingine ya Dola kwa usimamizi na uongozi shupavu, nikianza na wewe Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuongoza Bunge hili kwa umahiri na busara. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamisi Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania kwa uongozi makini wa Mhimili wa Mahakama unaozingatia, miiko,dira na dhima ya mhimili huo. Hakika uongozi wake umefanikisha upatikanaji wa HAKI kwa wanyonge na kujenga misingi imara ya utawala wa sheria hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, niruhusu pia kumpongeza Mheshimiwa Balozi Hussein Athman Kattanga kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma. Nampongeza kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa umakini na kwa weledi mkubwa. Vilevile, nawapongeza Mheshimiwa Othman Masoud Othman kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, napenda niwapongeze na kuwashukuru kwa dhati wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na Usalama. Kipekee, naomba niwatambue Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo; Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Nyakoro Sirro; Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athuman Msuya; Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee; Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala; Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, CP Salum Hamdun; Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Gerald Kusaya Musabila; na Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, John William Masunga. Utumishi wao uliotukuka na uzalendo wa hali ya juu umetuwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa amani Tunawaomba muendelee kutimiza wajibu wenu wa kulinda amani na usalama wa nchi yetu kwa moyo wa uzalendo.

Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati napenda kuipongeza na kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Sillo Daniel Baran, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Makamu wake Mheshimiwa Omar Mohamed Kigua, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kwa umakini wao katika kuchambua na kutoa maoni na ushauri ambao umesaidia kuboresha mapendekezo ya Bajeti hii. Aidha, ninawapongeza Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge za Kisekta kwa michango waliyotoa kupitia vikao vya Kamati za Kisekta iliyowezesha kuboresha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22.

Mheshimiwa Spika, ninawashukuru viongozi na watumishi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango na taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu ya kila siku hususan maandalizi ya bajeti hii. Kipekee ninamshukuru Mheshimiwa Hamad Y. Masauni, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni. Ninamshukuru sana Katibu Mkuu Hazina na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel M. Tutuba, pamoja na Naibu Makatibu Wakuu, Amina Kh. Shaaban, Adolf H. Ndunguru na Dkt. Khatibu M. Kazungu pamoja na watumishi wa kada zote wa Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, ninamshukuru Profesa Florens D. Luoga, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kwa kusimamia sekta ya fedha kwa weledi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, namshukuru Ndugu Alphayo J. Kidata, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi mkubwa. Kadhalika, namshukuru CPA Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi nzuri anayoifanya ya kukagua na kutoa taarifa za matumizi ya fedha za umma kwa wakati pamoja na kuishauri Serikali. Ninamshukuru CPA Athumani S. Mbuttuka, Msajili wa Hazina kwa kuendelea kusimamia Mashirika ya Umma na kuhakikisha Serikali inapata mchango na gawio stahiki. Ninamshukuru pia Dkt. Albina Chuwa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa kusimamia vizuri Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na kuendelea na maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza Mawaziri wenzangu na Naibu Mawaziri wote walioaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nyadhifa hizo. Aidha, niwapongeze pia wabunge wenzangu wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuaminiwa na vyama vyao na kuchaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha bungeni. Kwa moyo wa dhati napenda kumshukuru mke wangu mpenzi Bi Neema Nchemba, kwa kunitia moyo na kuniombea wakati wote ninapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yangu. Vile vile, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa dhati wapiga kura wangu wa Jimbo la Iramba Magharibi walioniamini na kunichagua tena kwa kishindo kuwa Mbunge wao. Ninawaahidi kuwa sitawaangusha.

Mheshimiwa Spika, niwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote ambao wameendelea kulipa kodi kwa hiari. Rai yangu kwao ni kuwa, tukitumia rasilimali za nchi yetu vizuri na kufanya kazi kwa umoja na bidii, tutaifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi na biashara sio tu kwa ukanda wa Afrika Mashariki bali kwa Afrika nzima. Vile vile, navishukuru vyombo vyote vya habari kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa dini kwa sala na dua zao zilizotuwezesha kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa amani na utulivu. Aidha, nawashukuru kwa kuliombea Taifa katika kipindi kigumu tulichopitia cha kuondokewa na viongozi wa kitaifa pamoja na mlipuko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya korona. Sala na dua zao zimetuwezesha kupita kwa amani katika kipindi cha mabadiliko ya uongozi wa kitaifa na hatimaye kumpata Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Ninawasihi waendelee kuliombea Taifa letu bila kuchoka.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa lakini si kwa umuhimu napenda nikushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news