BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MBUNGE EALA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA). Balozi Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa EALA leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam. Picha na Mambo ya Nje.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news