BILIONI 18/- KUKAMILISHA UPELEKAJI UMEME VIJIJI VILIVYOSALIA KONDOA

Veronica Simba na Hafsa Omar

Serikali imetenga kiasi cha takribani shilingi bilioni 18.6 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vijiji vyote 42 vilivyopo wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati akizindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili Ngazi ya Mkoa, uliofanyika Julai Mosi mwaka huu katika Kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa.

“Kijiji cha Itaswi ni moja kati ya vijiji 42 vilivyopo katika Wilaya ya Kondoa ambavyo hadi sasa bado havijafikiwa na huduma ya umeme. Hivyo basi, Serikali kwa kutambua hilo imetenga kiasi hicho cha fedha ili kukamilisha kazi hiyo,” alieleza Waziri.

Aidha, katika hafla hiyo, Dkt. Kalemani aliwatambulisha Wakandarasi watakaotekeleza Mradi husika wilayani humo, ambao ni kutoka Kampuni ya Ok Electrical and Electronics Service Ltd na kuwataka wananchi ambao hawajafikiwa na umeme kutokuwa na shaka kwani Serikali imejipanga vema kuhakikisha wote wanafikiwa na nishati hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati).

“Mkoa wa Dodoma kwa ujumla wake una vijiji 387 vyenye umeme kati ya 565 vilivyopo. Leo ninawakabidhi wakandarasi hawa kwenu wananchi ili kwa pamoja waushambulie Mkoa huu na kuhakikisha vijiji vyote 178 vilivyosalia vinapatiwa umeme,” alisisitiza.

Waziri aliwahamasisha wananchi kukamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao mapema ili Mkandarasi atakapofika katika maeneo yao, wawe tayari kulipia na kuunganishiwa umeme.

Aliwashauri wananchi wenye nyumba ambazo siyo kubwa, kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji kutandaza nyaya katika nyumba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo akipunga mikono kuwasalimu wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto).
Mbunge wa Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (Rural Energy Board – REB), Wakili Julius Kalolo, alieleza kuwa malengo ya Serikali ni kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vyote ifikapo Disemba 2022 na vitongoji vyote mwaka 2025.

Wakili Kalolo alieleza zaidi kuwa, utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, utaongeza uwekezaji wa miradi katika sekta mbalimbali vijijini ikiwa ni pamoja na kuanzishwa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.

“Aidha, miradi hii itaongeza ufanisi katika sekta ya madini kwa kufikisha umeme katika migodi ya wachimbaji wa madini hususani wachimbaji wadogo na wa kati,” alieleza Mwenyekiti.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Hamis Mkananchi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oswald Urassa (kushoto) na Louis Accaro (kulia), wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati) akiwasili katika eneo ilipofanyika hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma. Wanaomwongoza ni Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kulia) na Katibu wa Naibu Waziri wa Nishati, Mhandisi Ngereja Mgejwa (kushoto).
Mwakilishi wa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Ahmed Chinemba (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kulia), wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, Julai 1, 2021.
Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Ngazi ya Mkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Baadhi ya watoto ambao ni wakazi wa kijiji cha Itaswi, wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakiwa katika eneo ilipofanyika hafla ya kuzindua Mradi Kabambe wa kusambaza umeme vijijini, Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Kimkoa, Julai 1, 2021. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Mojawapo ya faida za umeme vijijini ni kuboresha kiwango cha elimu katika shule mbalimbali ambazo watoto kama hawa wanasoma kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga alieleza kuwa kuanzishwa kwa Wakala huo na utashi wa dhati wa Serikali, kumeleta mageuzi makubwa ya Sekta ya Nishati Vijijini ambapo upatikanaji wa umeme umeongezeka kutoka vijiji 518 sawa na asilimia 4 ya vijiji 12,268 mwaka 2007 hadi kufikia vijiji 10,312 sawa na asilimia 84 mwezi Machi, 2021.

Mhandisi Maganga alibainisha kuwa mafanikio hayo yamepatikana kufuatia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye Mfuko wa Nishati Vijijini (REF) kuanzia mwaka 2008, ambapo kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 3.5 zimewekezwa. Uwekezaji huo umewezesha utekelezaji wa miradi kufikia hatua ya vitongoji.

“Hadi sasa, umeme umefika katika Wilaya zote. Aidha, Kata 3,225 kati ya 3,956 sawa na asilimia 82 na Vitongoji 26,860 kati ya 64,384,” alibainisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya viongozi wilayani humo akiwemo Mkuu wa Wilaya, Hamis Mkananchi na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji walipongeza kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali katika kupeleka umeme vijijini, hususani katika Wilaya hiyo.

Hata hivyo, viongozi hao waliomba kazi ya kukamilisha upelekaji umeme katika vijiji vilivyosalia, itekelezwe kwa kasi ili kukidhi kiu ya wananchi ambao wamejiandaa kupokea nishati hiyo ili waitumie katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo hivyo kuboresha maisha yao.

Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali, Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini Mhandisi Francis Songela, Louis Accaro, Oswald Urasa na viongozi wengine mbalimbali pamoja na wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news