CCM Kinondoni yateua wagombea mitaa miwili, wajumbe watatu

Na Anneth Kagenda, Diramakini Blog

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni kimesema kuwa uteuzi wa wagombea wa chama hicho umemalizika vizuri kwa Halmashauri Kuu iliyoketi Julai 7, 2021 na kupata wagombea wa uenyekiti wa mitaa miwili pamoja na wajumbe watatu.
Akizungumza na DIRAMAKINI Blog jijini Dar es Salaam Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Sure Mwasanguti pamoja na Katibu wa Siasa na Uenezi wilaya, Joha Dolle wamesema kuwa uteuzi huo umeenda vizuri.

Katibu Mwasanguti, amesema uteuzi wa wagombea kwa nafasi hizo umeenda vizuri na kwamba wameteua Makada safi ambao anaamini baada ya kuchaguliwa kwenye kinyang'anyiro wataendelea kukiwakilisha vizuri chama.

"Wagombea wote walikuwa wanafaa na walikuwa na sifa, lakini alitakiwa mmoja na ndiye huyo aliyeteuliwa hivyo basi baada ya uchukuaji wa fomu za tume na kurudisha tutaanza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Agosti 1, 2021,"amesema.

Katibu Mwenezi Joha, amesema, "kwanza niwaombe wananchi wawachague wenyeviti wanaotokana na CCM kwani hata mitaa yote 106 ipo chini ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia waendelee kutuamini kwani kazi zinaonekana zilizofanyika na wala hazihadithiwi,"amesisitiza.

Aidha, mwenezi huyo amesema wenyeviti ambao wanaenda kuingia kwenye kinyanga'nyiro hicho ni pamoja na Thomas Leopard Kalunga kutoka Kata ya Msasani Mtaa wa Mikoroshini.

Ambapo mwenyekiti mwingine ni yule wa Kata ya Mikocheni Mtaa wa Darajani, Charles George Gupta huku wajumbe wakiwa ni watatu.

"Wajumbe watatu wa Serikali za mitaa yaani Viti maalum wawili na mchanganyiko 1, lakini pia fomu zinaanza kuchukuliwa Julai 10, 2021 na kurudisha ni Julai 10 hadi 16 /07/2021 na uchaguzi utakuwa Agosti 1, mwaka huu,"amesema Mwenezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news