CHADEMA Dodoma watangaza maandamano kushinikiza Freeman Mbowe aachiwe huru

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dodoma kimeazimia kufanya maandamano yasio na kikomo mpaka pale Mwenyekiti wa chama chao Taifa,Freemaan Mbowe atakapoachiliwa na Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo na jeshi la polisi jijini Mwanza akiwa hotelini siku moja kabla ya kwenda kwenye kongamano la kudai katiba mpya.
Akiongea na waandishi wa habari leo Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dodoma,  Mathias Nyakapala amesema, matendo ya unyanyasaji na uvunjwaji wa sheria bado yanaendelea nchini.

"Tunaotoa saa tano mwenyekiti wetu na viongozi wengine wawe wameachiliwa na jeshi la polisi tena bila masharti yoyote na kama hawatamuachia sisi CHADEMA Dodoma tumeazimia kufanya maandamano yasio na kikomo kesho saa mbili asubuhi na tutaanzia hapa katika ofisi zetu za Kanda zilizopo hapa Area C," amesema Nyakapala.

Ameongeza kuwa, "Kwa muda mrefu Mwenyekiti wetu haikujulikana yuko wapi kumbe wamemkamata Mwanza na kumpeleka jijini Dar es Salaam na kwenda kupekuwa nyumbani na vyumba vya watoto na kuchukuaa kompyuta mpakato za watoto, huu ni udhalishaji na haya matendo sio ya kuyafumbia macho, " amesema.

Hata hivyo,amesema baadhi ya viongozi wa chama hicho wameendelea kukamatwa bila makosa yoyote waliyoyafanya.

"Maandamano haya ni maazimio yetu sisi wana CHADEMA Dodoma tunataka Mwenyekiti na viongozi wengine waachiwe huru na tutaazimia kuandama nchi nzima endapo wataendelea kuwachukua viongozi wetu ikumbukwe Mbowe ni kiongozi wa chama Taifa hivyo tutafika wanachama wa CHADEMA wote kama hawatamuachia, " amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news