Italia yatwaa Ubingwa Euro 2020

Na GODFREY NNKO

Italia na England zimetoshana nguvu kwa dakika 120 kwa kutoka sare ya moja kwa moja.
Baada ya sare hiyo ndani ya dimba la Wimbley nchini Uingereza mikwaju ya penaliti ilitumika kuamua matokeo katikati mtanange huo wa fainali.

Hali hiyo ilififisha matumaini ya timu ya taifa ya England ya kubeba ubingwa wa Euro 2020.

Ni baada ya Italia kuwadunga mikwaju ya penati 3-2.

England ambayo ilikuwa inahitaji kumaliza ukame wa taji baada ya miaka 55 unaweza kusema mkosi wa kocha Gareth Southgate wa kukosa penati umeendelea maana alikosa akiwa mchezaji, amekosa kama kocha.

Pamoja na mlinda mlango Jordan Pickford wa Everton kufanya kazi nzuri bado kukosa kwa Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka kulionyesha kuwa hakuna alichokifanya kwani mwisho wa siku alipoteza.

Licha ya kucheza nyumbani Wembley mbele ya mashabiki 60,000 bado haikutosha kuwa mabingwa.

England walikuwa wa kwanza kuandikisha bao kupitia kwa beki wa Manchester United Luke Shaw akimalizia krosi majanga ya Kieran Trippier wa Atletico Madrid.

Ni kabla ya Italia kusawazisha bao hilo kupitia kwa Leonardo Bonucci ungwe ya pili baada ya piga nikupige langoni mwa Three Lions.

Italia wanafikisha mechi 34 bila kupoteza miongoni mwa rekodi bora ngazi ya taifa. Ushindi huu ni wa kipekee kwa Italia tangu mwaka 1968.

Post a Comment

0 Comments