Jimbo la Lushoto lapewa Bilioni 4/- za maendeleo

Na Yusuph Mussa, Lushoto

JIMBO la Lushoto mkoani Tanga limepata sh. bilioni nne (4) katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya ujenzi wa barabara, ambapo sh. bilioni 3.5 ni kwa ajili ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe kutoka Mlalo-Ngwelo-Mlola-Makanya-Milingano hadi Mashewa yenye urefu wa kilomita 70, huku sh. milioni 500 zikitumika kutengeneza barabara maeneo korofi.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi 'Bosnia' akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mdando, Kata ya Makanya, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Ni baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi maarufu kama 'Bosnia' kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mdando, Kata ya Makanya, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto, na kuwataka wakulima kutumia fursa hiyo wa ujio wa barabara ya uhakika kuweza kulima mazao kwa wingi na kupeleka sokoni.

"Jimbo la Lushoto tumepata bahati kubwa baada ya Serikali kutupatia sh. bilioni nne (4) kwa ajili ya ujenzi wa barabara, ambapo sh. bilioni 3.5 ni kwa ajili ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe kutoka Mlalo-Ngwelo-Mlola-Makanya-Milingano-Mashewa yenye urefu wa kilomita 70. Tukumbuke utengenezaji wa barabara hiyo sio kwa ajili ya maeneo korofi, bali barabara yote kuanzia mwanzo hadi mwisho inawekwa changarawe.

"Lakini tuzidi kumuombea na kumshukuru Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Tanzania), kwani pamoja na sh. bilioni 3.5, bado ametupa sh. milioni 500 ziitakazotumika kutengeneza barabara maeneo korofi. Niwaombe wakulima wenzangu, tumieni fursa hii ya barabara kuweza kulima mazao kwa wingi hasa maharage, kwani kutokana na kufunguka kwa barabara, wafanyabiashara wakubwa watakuja wenyewe kuchukua mazao yenu badala ya kuwatumia wachuuzi" alisema Shekilindi.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi 'Bosnia' akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mdando, Kata ya Makanya, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Ni baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi 'Bosnia' akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mdando, Kata ya Makanya, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto. Ni baada ya kumaliza mkutano wa hadhara. Shekilindi aliwahakikishia wananchi wa Kata ya Makanya kuwa tatizo la maji litamalizika, kwani kuna mradi mkubwa wa maji wa kata 13 wenye thamani ya sh. bilioni 16, ambapo usanifu na upembuzi yakinifu umeshafanyika, hivyo mradi huo utakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa kata 13 kati ya kata 15 za Jimbo la Lushoto.

Alisema vijiji vyote vitano vya Makanya vitapata umeme, na kila kijiji kitapata nguzo 20 kwa awamu ya kwanza, na baadae vitongoji vyote vya kata hiyo vitapata umeme, huku akiwakumbusha wananchi kuwa bei ya kuingiza umeme kwenye nyumba ni sh. 27,000, hivyo asije akatokea mtu akasema kunatakiwa sh. 200,000 ama 400,000 kwa ajili ya kupeleka nguzo karibu na nyumba za wateja.

Shekilindi ameahidi kuwapelekea Kituo cha Afya Makanya ambacho kitakidhi haja ya wananchi hao kuweza kupata huduma ya afya, huku akiwataka kukaa pamoja na kukubaliana kitajengwa wapi. Na wakati wakiweka mipango hiyo, ameahidi kukamilisha zahanati za Mdando na Bombo kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo na nguvu za wananchi, amnapo Zahanati ya Mdando atapeleka bati 27 ili kukamilisha upauaji, halafu wakamilishe umaliziaji.
Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga Shaaban Shekilindi 'Bosnia' katika Kijiji cha Mdando, Kata ya Makanya, Tarafa ya Mlola wilayani Lushoto.(Picha na Yusuph Mussa).

Shekilindi, pia ameahidi Serikali kujenga bwawa kwa ajili ya umwagiliaji Kata ya Makanya, kwani maji mengi yanayopita kwenye mto ya kata hiyo yanapotea bure kwa kwenda kuingia baharini bila kunufaisha wananchi kiuchumi. Hivyo kama maji hayo yatajengewa bwawa, itasaidia kwa kilimo, na kupata maji safi na salama.

Post a Comment

0 Comments