Kelvin wa Mbezi Beach naye anusurika kifo baada ya mpenzi wake Tina kuchoma nyumba moto

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Siku chache zikiwa zimepita baada ya mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Khamisi maarufu Zungu kufariki dunia baada ya mpenzi wake Neema Mushi waliokuwa wanaishi naye Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam, kuchoma moto nyumba na kusababisha kifo kwa kile kinachodaiwa wamepishana kauli, huku fremu za wafanyabiashara zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea moto. Tukio lingine limetokea leo Julai 26,2021.

Ni baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kuchoma moto nyumba ya mpenzi wake aliyetambulika kwa jina moja tu la Kelvin.
Dada huyo aliyetambulika kwa jina la Tina amefanya tukio hilo leo huku wivu wa kimapenzi ukitajwa kusababisha hasara hiyo kubwa.

Imeelezwa kuwa, Mwanaume huyo hakuwa ndani wakati mpenzi wake huyo akiichoma nyumba hiyo, hivyo hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha kwenye tukio hilo.Mashuhuda wamemweleza MWANDISHI DIRAMAKINI kuwa, Tina ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach aliruka ukuta na kuingia nyumba ya Kelvin, lakini baada ya kuwasha moto alishindwa kutoka ndipo akapiga kelele kuomba msaada wa kuokolewa.

Post a Comment

0 Comments