KMC FC KUMALIZA LIGI KESHO NA IHEFU UWANJA WA UHURU

Kikosi cha KMC FC hapo kesho kitashuka kwa mara ya mwisho katika msimu huu wa Ligi kuu soka Tanzania bara kwa kuwakaribisha Timu ya Ihefu kutoka Mbarali mkoani Mbeya mchezo utakaopigwa saa 16:00 jioni katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.
KMC FC ambao ni wenyeji katika mchezo huo, hadi sasa mandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa chini ya Makocha , Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo kocha msaidizi ikiwa ni kukiweka vizuri kikosi hicho na hivyo kuhakikisha kwamba ushindi unapatikana na hivyo kujihakikishia kumaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/2021 katika nafasi ya tano.

Katika mchezo wa awali ambao ulipigwa katika Dimba la Hailand State Ubaruku Mbalali , KMC FC ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli moja kwa bila na kwamba mchezo wa kesho kikosi kimejiandaa kufanya vizuri licha ya kwamba kutakuwa na ushinda mkubwa.

Tunapambana kumaliza ligi kwenye nafasi ya tano hivi sasa, hivyo mchezo hautakuwa mrahisi hasa ukizingatia ndio tunakwendakucheza mechi ya mwisho kwa msimu huu, lakini tupovizuri na tumejipanga zaidi kuhakikisha kwamba kama Timu tunashinda mchezo wetu na alama tatu zinabaki mikononi mwa Manispaa ya Kinondoni.

Aidha, Mashabiki wetu tunawaomba mjitokeze kwa wingi kutoa sapoti kwa wachezaji wenu, wamefanya kazi kubwa katika msimu huu na hivyo kesho tunakwendakumaliza ligi kwakujenga heshima kubwa kwenye Kblabu yetu, na sisi hatuta waangusha , tutakwenda kushinda kwa kishindo, wachezaji wanamorali nzuri, makocha wamefanya kazi kubwa ya kukiandaa kikosi hivyo mjitokeze kuwaunga mkono.

Hata hivyo katika mchezo wa 33, KMC FC iliibuka na ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya JKT Tanzania ambao ulipigwa Julai 15 katika Dimba la Uhuru hapa Jijini Dar es Salaam na hivyo kuiwezesha timu kufikisha alama 45 na kupanda hadi kwenye nafasi ya tano mwa msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Imetolewa leo Julai 17

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC

Post a Comment

0 Comments