🔴LIVE:Rais Samia akiwaapisha Mabalozi wateule leo Julai 27, 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha mabalozi 13.

Uapisho huo umefanyika leo Julai 27,2021 Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kuwateua.

Mheshimiwa Rais amesema kuwa, huu ni uteuzi wa vijana na wengi wao wapo chini ya miaka 45.Unaweza kusoma: Rais Samia Suluhu Hassan ateua mabalozi

"Hatujawapa mkale ujana, bali sasa ni imani yetu mtakuwa wepesi zaidi kuliko wazee. Pia tumechukua kutoka maeneo tofauti, fani tofauti.

"Niwape hongera na nina uhakika kazi iliyo mbele yenu mtaiweza tu. Kuteuliwa kwenu kunaonyesha kwa viwango vya uaminifu mmevionyesha kwa serikali yenu. Wakati ninawapongeza mkumbuke mna majukumu makubwa mbele yenu. Toka nimekuwa Rais nyie ndio mabalozi wa kwanza ninawateua, kazi iendelee, msiniangushe.

"Dunia yetu leo inakumbwa na janga la Covid-19, asubuhi ya leo tulikuwa na Mkurugenzi wa CDC na akasema ndani ya jumuiya kuna misaada mingi kwa ajili ya Covid, lakini sijasikia kutoka kwenu, mjifunze kutafuta kwa ajili ya nyumbani.Unaweza kusoma hapa; Rais Samia Suluhu ateta na Mkurugenzi wa CDC Afrika

"Kuhudumia ofisi ya kidiplomasia ni gharama, lakini tunafanya kushirikiana na wengine na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini, tunabadilisha sera za uwekezaji,"amesema Rais Samia.

Akizungumzia kuhusiana na tozo za miamala ya simu, Rais Samia amesema kuwa, "Tulianza huu mfumo Julai, lakini wananchi walilalamika na tulitumia kama wiki na baadae nikawataka mawaziri wawili wakae walifanyie kazi, tunatarajia maoni ya kamati keshokutwa.

"Tuliyaweka kwa nia njema, njia za vijijini hakuna na sehemu kubwa ya fedha hii itaenda kwenye njia za vijijini, wakulima wasiozewe na mazao pia kwenye maji.Tumesikia vilio lakini tozo zipo, tutaangalia njia nzuri,"amebainisha Rais Samia.

Wakati huo huo, Rais Samia amezungumzia kuhusiana na kilio cha kupanda bei ya mbolea amesema, Serikali inalifanyia kazi suala hilo na suluhisho litapatikana karibuni.

Awali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberatus Mulamula alimshukuru, Rais Samia kwa imani kubwa ambayo amewekeza kwao.

Balozi Mulamula amesema, ameishi katika wizara hiyo kwa miaka mingi na hakumbuki kama ilishawahi kutokea hivyo.

Amesema,  mabolozi sita kati ya walioapishwa leo ni wanawake, hivyo uwiano wa kijinsia umezingatiwa na wengi wao wana umri chini ya miaka 45 na teuzi zimengatia pande zote za Muungano na wapo mabolozi wametoka nje ya wizara kuleta utaalamu na uzoefu tofauti.

Waziri Mulamula amesema, wizara kwa sasa inaongozwa na wanadiplomasia na amewafilisi visingizio.

Amesema wakati Rais Samia anakutana na mkurugenzi wa CDC leo, ameelezea umuhimu wa diplomasia ya afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news