🔴LIVE:Simba SC vs Yanga SC Fainali ya Azam Sports Federation Cup 2021/21

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Simba SC wamefanikiwa kutetea Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Thadeo Lwanga dakika ya 80 ndiye aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimafaifa wa Msumbiji, Jose Luis Miquissone.

Yanga ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 baada ya kiungo Mkongo, Tonombe Mukoko kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.

Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu
Kikosi cha Simba SC kitakachoanza leo Julai 25,2021 dhidi ya Simva, fainali ya Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma mwisho wa reli
Kikosi cha Yanga SC kitakachoanza leo Julai 25,2021 dhidi ya Simva, fainali ya Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma mwisho wa reli.

Post a Comment

0 Comments