Makamu wa Rais Dkt. Mpango akagua miradi ya maendeleo wilayani Kakonko

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa ziarani mkoani Kigoma hii leo Julai 18, 2021 ametembelea wilaya ya Kakonko ili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Akiwa kijijini Kasanda, Makamu wa Rais amepokea changamoto ya vijana wa eneo hilo kushindwa kupata ajira katika mradi wa ujenzi wa barabara licha ya kwamba mradi huo unatekelezwa katika maeneo yao. Makamu wa Rais amesema serikali ilikwisha kutoa muongozo kwa wakandarasi kuzingatia ajira kwa wazawa na kumuagiza Naibu Waziri wa Ujenzi mhandisi Godfrey Kasekenya kulifuatilia suala hilo na kupata ufumbuzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasanda wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani humo Julai 18, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali katika eneo la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko mara alipowasili kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Dkt. Joseph Edward juu ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo.

Amewashukuru wananchi wa Kasnada kwa kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidi na kutumia fursa zitakazopatikana mara baada ya mkoa wa Kigoma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme kujiletea maendeleo.

Aidha Makamu wa Rais ameweka jiwe la msingi Hospitali ya wilaya ya Kakonko ilioanza kwa ujenzi wa majengo saba yanayogharimu shilingi Bilioni 1.8 na kutarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka jiwe la msingi Hospitali ya Wilaya ya Kakonko Julai 18,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kakonko waliojitokeza kumsikiliza wakati wa uwekaji jiwe la msingi Hospitali ya Wilaya hiyo Julai 18,2021.

Makamu wa Rais ameagiza wizara ya fedha kurejesha kiasi cha fedha shilingi milioni 187.7 zilizochukuliwa na mfuko mkuu wa serikali wakati wa kufunga mwaka wa fedha 2019/2020 ili zitumike katika kukamilisha miundombinu mingine ya hospitali hiyo. Makamu wa Rais ameagiza fedha zinazoletwa katika mradi huo kuhakikisha zinatumika vizuri na thamani ya fedha ilingane na matokeo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika uwekaji wa jiwe la msingi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amewahimiza wananchi wa Kakonko kuendelea kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Amewahakikishia kwamba serikali ya awamu sita iataendelea kuboresha huduma za jamii katika wilaya hiyo na kutekeleza ahadi zilizoahidiwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news