Makamu wa Rais Dkt.Mpango atembelea Bandari ya Mtwara

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametembelea Bandari ya Mtwara na kujionea ujenzi wa gati mpya uliofanywa bandari hapo kwa kugharimu shilingi bilioni 157.
Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isidor Mpango ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara na maandalizi ya TPA kuhudumia shehena ya Korosho ambayo itapita yote katika bandari hiyo msimu huu unaoanza mwezi Septemba kama ilivyoelekezwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan. Pichani Mhe Makamu wa Rais akipata maelezo kuhusu bandari ya Mtwara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Eric Hamissi.

Akiwa bandarini hapo Julai 26,2021 Mkamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha kuwa Bandari ya Mtwara inatumika ipasavyo ili kuinua uchumi wa mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla. Ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Bandari kuendelea kutafuta masoko katika nchi jirani kama vile Msumbiji, Malawi na Comoro ili kuongeza wigo wa matumizi ya bandari ya Mtwara na kuliongezea taifa mapato.
Aidha

Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Kilimo, kuhakikisha mazao yote yanayolimwa Mikoa ya Kusini ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kama vile mbaazi,ufuta na Korosho yasafirishwe kupitia Bandari ya Mtwara badala ya Bandari ya Dar es Salaam kuanzia msimu ujao.

Aidha ameitaka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ujenzi na uchukuzi kuhakikisha kwamba pembejeo za korosho zinapitia Bandari ya Mtwara na siyo bandari ya Dar es Salaam na utaratibu huu kuwa wa kudumu kuanzia sasa.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho amesema tayari bandari hiyo ipo tayari kupokea meli zote zinazobeba shehena ya mizigo kwaajili ya mikoa ya kusini nan chi jirani na tayari wanafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali ili kuzishawishi kutumia bandari hiyo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ametembelea na kuweka jiwe la msingi mradi wa chujio la maji Mangapa unaogharimu shilingi bilioni 2.3. Mradi huo unatarajiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama mkoani Mtwara.

Makamu wa Rais ameagiza mradi huo kukamilika mwezi Septemba kama ilivyopangwa hapo awali ili wananchi waanze kupata maji safi na salama. Aidha ameagiza wizara ya maji kutumia malighafi za ndani ya nchi katika ujenzi wa miradi mbalimbali hapa nchini. Ametolea mfano suala la chokaa kuchukuliwa kutoka nje ya nchi halitakiwi kupewa kipaumbele kwani yapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news