Mchepuko wa Staa wa Muziki Grand P wavunja penzi lililokolea na Mrembo mwenye umbo matata

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mrembo matata wa Ivory Coast, Eudoxie Yao na nyota wa muziki raia wa Guinea, Grand P wamehitimisha mahusiano yao baada ya Grand P kudaiwa kuchepuka na pisi kali nyingine.
Eudoxie Yao amedai kuwa  Grand P amekuwa si mwaminifu, kwani licha ya kumtimizia kila kitu amekuwa akiwafungulia moyo wake warembo wengine baada ya kunaswa akila bata.

Baada ya tangazo la Mrembo huyo la kuhitimisha mahusiano yao, baadae mambo yalianza kubadilika, kwa kusambaa kwa picha za mpenzi wake akila bata katika viwanja vikali.
Inasemekana, Grand P amekuwa si mwaminifu kwani, tabia ya kujiachia viwanja tofauti na warembo imekuwa kama starehe yake ya kwanza, hivyo kumwachia sonona mpenzi wake.
Picha zinazohusiana na tukio la mwanamke ambaye amekuwa akila naye bata zimesambaa mitandaoni kama ifuatavyo;

Post a Comment

0 Comments