Msemaji Mkuu wa Serikali atoa msimamo, ataka wapuuzwe

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Serikali haijatoa maelekezo ya kuwalazimisha watumishi wa umma kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Korona (Uviko-19) kama ambavyo imezushwa na wahalifu kupitia mitandao ya kijamii.
 
Hayo yamesemwa leo Julai 29, 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo za upotoshaji.

Wananchi wakiwemo watumishi wa umma puuzeni uzushi huo.Na endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka Serikalini kupitia kwa viongozi na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu juu afua mbalimbali za kujikinga na Uviko-19.

 

Msimamo wa Serikali ni kuwa utoaji wa chanjo ya Uviko-19 unafanyika kwa hiari ya mtu yeyote atakayekuwa tayari kupokea chanjo hiyo. Na kwa kuanzia makundi yatakayopewa kupaumbele ni watumishi wa afya (Madaktari na Wauguzi), Watu wenye magonjwa sugu, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na Askari waliopo katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Serikali inawataka wanaofanya uhalifu huu wa kuzusha, kufanya uchochezi na kuwatisha wananchi kuacha mara moja kwa kuwa ni makosa kisheria.

Aidha, Wananchi wote endeleeni kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa na wataalamu wa afya zikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka na sabuni, kuvaa barakoa, kujiepusha na misongamano isiyo ya lazima na kuzingatia umbali usiopungua mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Kwa hivi sasa Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya kutoa chanjo katika Mikoa 10 itakayoanza kutoa chanjo kwa wananchi na utaratibu utakapokamilisha mtajulishwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news