NHC YATAKIWA KUBUNI MIRADI MIPYA MOROGORO

Na Munir Shemweta, MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Tifa (NHC) mkoa wa Morogoro kubuni miradi mipya ya ujenzi wa katika mkoa huo ili kuliwezesha shirika kuingiza fedha badala ya kutegemea nyumba za zamani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Morogoro alipotembelea ofisi za shirika hilo akiwa katika ziara ya kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa wa Morogoro jana.

Dkt.Mabula alitoa kauli hiyo jana mkoani Morogoro wakati akizingumza na watumishi wa ofisi ya shirika hilo mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa huo.

Amesema, haileti maana NHC kutegemea nyumba zake zilizojengwa na mkoloni bila ya kuwa na mipango mipya ya ujenzi itakayowezesha shirika hilo kuwa na nyumba nyingine za kisasa zitakazoliwezesha shirika kujiongezea kipato.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Morogoro alipotembelea ofisi za shirika hilo akiwa katika ziara ya kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa wa Morogoro jana. Wa pili kushoto mstari wa mbele ni Meneja wa NHC Morogoro, Constantine Yuda.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mkoa wa Morogoro bado una uhitaji mkubwa wa nyumba zikiwemo zile za kupangisha hasa kwenye maeneo mapya na kusisitiza kuwa NHC haina budi kuongeza kasi kwa kubuni miradi mipya itakayosaidia shirika kuongeza kipato.

‘’Kumbe ninyi bado mkoa kizamani yaani hamna mradi wa ujenzi wa nyumba mpya na mnategemea zile za zamani? Mnatakiwa kujiongeza kwa kubuni miradi mipya ili muweze kuongeza mapato ya shirika,’’ amesema Dkt Mabula. Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula alimtaka Meneja wa NHC Morogoro Constantine Yuda kwenda katika halmashauri za mkoa huo ili kupatiwa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miradi mipya ikiwemo ya nyumba za watumishi kwenye halmashauri za mkoa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news