Rais Samia afungua Kongamano la Kumbukizi ya Mwaka mmoja wa Hayati Benjamin Mkapa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Rais Mtaafu wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa alikuwa kiongozi wa tofauti kwani alikuwa jasiri, shupavu, imara, mpenda maendeleo, mwanadiplomasia aliyekuwa na maono makubwa ya ndani na nje ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo Julai 14,2021 kwa ajili ya kufungua Kongamano la kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (1St Mkapa’s Legacy Symposium).

Akizungumza leo, Jijini Dar es samaam katika Kongamano la Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa Hayati Mkapa, Rais Samia alisema kwamba kitabu cha historia ya Tanzania hakiwezi kukamilika bila kuwepo kwa sura nzima yenye kumwelezea Hayati Mkapa na magezi mengi aliyoyafanya katika uongozi wake.

“Kitabu cha historia ya Taifa letu hakiwezi kukamilka bila kuwepo kwa sura nzima itakayomwelezea Hayati Mzee Mkapa, sio tu kwasababu alikuwa Rais wetu, lakini pia kutokana na mageuzi makubwa aliyoyafanya kwenye nchi yetu. Alikuwa mtu wa kipekee sana, mara zote ukikutana nae utaondoka umechota maarifa mengi”, alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema kwamba Hayati Mkapa ndie alienzisha taasisi nyingi nchini ambazo bado zinaendelea kufanya kazi nzuri mpaka leo. Akizitaja baadhi ya Taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB) pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF). Taasisi nyingine ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKURABITA) na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo Julai 14,2021 kwa ajili ya kufungua Kongamano la kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (1St Mkapa’s Legacy Symposium).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa na ule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo Julai 14,2021 kabla kufungua Kongamano la kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (Mkapa’s Legacy Symposium).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (1St Mkapa’s Legacy Symposium) katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa maendelea ya uchumi wa nchi kwa ujumla Rais Samia alisema kwamba Hayati Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza deni la Taifa kutoka asilimia 143.7 mwaka 1995 hadi asilimia 60.7 mwaka 2005 akichochewa na uwezo wake wa kidiplomasia katika kuzishawishi Taasisi za kifedha za Kimataifa na Nchi wahisani kusamehe madeni kwa kutumia mpango wa Heavily Indebted Poor Countries (HIPC) uliosimamiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Ukiachilia mbali shughuli hizo alizozifanya nchini, Hayati Mzee Mkapa pia alikuwa nguzo hata katika Mataifa mengine ambapo alisimama kidete katika kusuluhisha migogoro baina nchi na nchi kama ule mgogoro wa Burundi, lakini pia alishiriki midaharo ya Kimataifa na kutetea kile alichokiami mafano masuala ya utandawazi alikuwa mstari wa mbele kujipambambanua kwamba Dunia ya sasa ni ya utandawazi.

Kongamano hilo lilijumuisha mdahalo ambao uliwahusisha wanataaluma ngulia wa masuala ya Afya Duniani, akiwemo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro, mwakilishi wa Mambo ya Afya wa Shirika la Maendeleo la Marekani Balozi Dkt. Donald Wright, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bwn. Sanjay Rughani pamoja na Mtaalam Mwandamiazi wa Masuala ya Afya na Jinsia, Dkt. Fatma Mrisho, Rais Samia alisema amefurahishwa na mjadala huo ambao ulilenga kwenye masuala ya Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Harambee kwa ajili ya kuchangia Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF Endowment Fund) kwenye hafla ya kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (1St Mkapa’s Legacy Symposium) katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tunzo ya Picha kwa Mama Anna Mkapa kwa kutambua Mchango Mkubwa wa Hayati Mzee Mkapa alioutoa kwa Taifa, kwenye kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa (1St Mkapa’s Legacy Symposium) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo Juni 14,2021.(Picha na Ikulu).

“Nimefurahishwa sana na mdahalo huo, kwa kuzingatia Serikali ipo kwenye mpango wa kuanzisha Bima ya Afya kwa wote. Wataalamu wetu wa Afya wako hapa, natumai wameyasikia na kuayachukua ili kuyafanyia kazi’.

Rais Samia ameipongeza Taasisi ya Benjamin Mkapa chini ya uongozi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Ellen Mkondya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Adeline Kimambo kwa kuandaa kongamano hilo lililoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Wakfu ambapo Rais Samia aliahidi Serikali itachangia mfuko huo. Aidha, Rais amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuendeleza mambo mazuri yanayoachwa na viongozi wa Kitaifa pindi wanapofariki kama njia ya kuwaenzi na kurithisha vizazi vijavyo tunu ambazo nchi yao imebarikiwa nazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news