Rais Samia aipongeza Burundi kwa kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Burundi kwa kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa nchi hiyo huku wakiendelea kudumisha amani.

Pia, Mheshimiwa Rais Samia amempongeza Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye kwa jitihada zake za kukuza amani, demokrasia na uchumi.

Hayo yamesemwa leo Julai Mosi, 2021 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasilisha salamu za Rais Samia katika sherehe za maadhimisho hayo jijini Bujumbura. Burundi ilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962.

“Nipo mbele yako nikimuwakilisha Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia. Rais amenituma nilete salamu zake kwako kwamba anawapongeza sana Wana-Burundi kwa kuendelea kukuunga mkono.”

Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia amemuhakikishia Rais wa Burundi kwamba ataendeleza uhusiano wa kindugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili na pia ameahidi kuitembelea Burundi.

Kwa upande wake, Rais wa Burundi Mheshimiwa Ndiyashimiye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wana-Burundi waendelee kushikama na kushirikiana katika kuboresha maendeleo ya nchi yao. “Burundi itajengwa na Warundi wenyewe.”

Amesema kwa sasa wanajivunia hali ya amani na ulivu uliopo Burundi, hivyo amewataka wananchi wa nchi hiyo waendelee kushikamana na wasikubali kulisaliti Taifa lao.

WAZIRI MKUU ALIPOWASILI BURUNDI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokelewa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura, akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura na akipokelewa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza (kulia), akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza, akiwa katika ziara ya siku moja nchini Burundi Julai 01, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news