Rais Samia ateua Mkurugenzi wa TANROADS na Mwenyekiti wa TAFICORais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo;

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili kama ifuatavyo-

  1. Amemteua Bwana Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Bwana Mativila anachukua nafasi ya Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

  • Amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Kabla ya uteuzi huo Prof. Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.

 Uteuzi huo umeanza tarehe 28 Julai, 2021.

Post a Comment

0 Comments