RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI BURUNDI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais Samia Suluhu kesho Julai 16, 2021 anatarajia kuanza ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inaeleza kuwa Rais Samia akiwa nchini humo atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Ndayishimiye, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la Wafanyabishara wa Burundi na Tanzania kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Burundi.

Post a Comment

0 Comments