RC Kafulila apiga marufuku mikutano, mikusanyiko

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amepiga marufuku mikutano yote isiyokuwa na ulazima pamoja na mikusanyiko kwenye mkoa huo kwa kile alichoeleza ni katika kupambana na ugonjwa wa Corona.
Kafulila amepiga marufuku hiyo kuanzia Julai 24,2021 wakati wa kikao chake na viongozi wa dini pamoja na waganga wa tiba asili kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi yake.

Amesema kuwa, kama mikutano hiyo isipofanyika hakutakuwa na athari yeyote, basi isifanyike ndani ya mkoa huo kuanzia sasa kama moja ya njia ya kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha, kiongozi huyo ameagiza kweye magari ya kubeba abiria yakiwemo mabasi makubwa kwenye stendi zote za magari, kila abiria anatakiwa kuvaa barakoa ikiwemo kwenye stendi zote mkoani humo kuwepo kwa sabuni na maji tiririka.

"Kila abiria ambaye atakuja stendi, lazima avae barakoa kabla ya kuingia kwenye gari, lakini katika stendi zote kuwepo maji tiririka pamoja na sabuni, lakini ni marufuku abilia kusimama kwenye basi, magari yote yawe level seat," amesema Kafulila.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kwenye mkoa huo, ambako kutatokea msiba wasika msibani na ikiwezakana mara baada ya mazishi kusiwepo na matanga.

Aidha, amewataka wananchi kujenga tabia ya kula vyakula lishe au mlo kamili, huku akisisitiza mazoezi ya mara kwa mara kwani yanasaidia kupambana na ugonjwa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news