Serikali yawataka viongozi na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kufanya kazi kwa ufanisi

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.Dorothy Gwajima amewataka viongozi na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) kufanya kazi kwa weledi,uadilifu na uzalendo wa hali ya juu ili kuleta tija katika Taifa.
Waziri huyo ameyasema leo Julai 10,2021 jijini Dodoma wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO).

Amewataka kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya waliowachagua na jamii ya watanzania kwa ujumla.

"Napenda kuwasilisha nimepokea kwa mikono miwili taarifa ya kamati ya mpito kwani nimeisikiliza mapendekezo ya kamati ambayo wengine utekelezaji wake unahitaji kujitoa kwenu kwa hali na mali na mengine ni ya kwetu upande wa wizara," amesema Dkt. Gwajima.

"Ikumbukwe kwamba Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni chombo cha uwakilishi na kiungo muhimu kati ya mashirika na Serikali, hivyo kutofanyanyika kwa uchaguzi na kutokuwepo kwa baraza kihalali kulisababisha vyombo vya usimamizi wa mashirika ya kiserikali kushindwa kuteleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria,"amesema.

Amesema, "nikiwa kama msimamizi wa sheria na kanuni za mashirika yasiyo ya kiserikali nisingeweza kuvumilia vitendo vya ukiukwaji wa sheria na kanuni hizo,"amesema.

Hata hivyo, amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakitekekeza miradi na afua katika maeneo mbalimbali ya kiutekelezaji ikiwa ni pamoja na sekta ya afya,kilimo, elimu, maji, mazingira, utawala bora, nishati,uhifadhi wa jamii,uwezeshaji wa jamii na sekta nyingine.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Uratibu na Usimamizi wa Uchaguzi wa (NaCoNGO), Flaviana Charles amesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan na waziri wake kwa kuhakikisha uchaguzi wa NaCoNGO unafanyika.

Amesema, "mchakato wa uchaguzi uliofanyika kwa kufuata kanuni sheria na demokrasia licha ya ufinyu wa muda uliokuwepo lakini tumefanikisha jambo hili.

"Kama kamati ya mpito tunaenda kutoa mapendekeza baraza lipange ratiba ya uchaguzi mapema kabla ya miaka mitatu ili wadau wote waweze kujua ratiba sahihi ya uchaguzi ujao," amesema.

Naye Mwenyekiti mpya wa NaCoNGO, Lilian Badi amesema mchakato wa uchaguzi haukuwa rahisi kwani ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na muamko wa NGO,s katika ngazi zote za wilaya Mkoa hadi Taifa.

"Sasa kazi iendelee kwani NaCoNGO hii ni kisayansi,uweledi,utendaji na uwajibikaji mengi tumeyaona na sasa tunakwenda kuyafanyia kazi kwa kuimarisha mahusiano mazuri kati ya NGO,s na serikali," amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news