TDB YAKABIDHI VYOO VYENYE MATUNDU 20 KWA SHULE YA MSINGI IFWAGI MKOANI IRINGA

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya TPB, imekabidhi vyoo vyenye matundu 20 kwa shule ya msingi Ifwagi Halmashauri ya Mufundi mkoani Iringa Julai 05 Mwaka huu .

Akizungumza wakati wa kukabidhi Majengo hayo Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Benki ya TPB amesema TPB msaada huo ni sehemu ya TPB kurudisha faida kwenye jamii kutokana na kuiunga mkono benki hiyo.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Benki ya Tpb ,Diana Mnyonga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Majengo ya vyoo yenye matundu 20 katika shule ya msingi Ifwagi Halmashauri ya Mufundi Mkoani Iringa yaliyojengwa na Benki ya Tpb hafla iliyofanyika Julai 05,2021.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Benki ya Tpb ,Diana Mnyonga akifungua kitamba cha jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa Majengo ya vyoo yenye matundu 20 yaliyojengwa na Benki ya Tpb katika shule ya Msingi Ifwagi Halmashauri Mufindi Mkoani Iringa ,hafla iliyofanyika Julai 05 Mwaka huu .
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ifwagi Halmashauri ya Mufundi Mkoani Iringa wakionesha furaha yao mara baada ya kukabidhiwa majengo ya vyoo yaliyojengwa kwa msaada wa benki Tpb na kukabidhiwa shuleni hapo Julai 05 mwaka huu.

Myonga amesema kuwa richa ya kuikabidhi majengo hayo pia benki hiyo itatoa samani za ofisi za walimu ambazo waliomba shule kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi shuleni hapo

aidha ametaja baadhi ya maeneo ambayo TPB wamekuwa wakitoa msaada kuwa ni pamoja na sekta ya afya kwa kutoa vifaa tiba, mashuka magodoro na sekta ya elimu ambapo husaidia kutoa madawati, viti, meza na kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya shule na vituo vya afya.

Pia ametoa rai kwa wanafunzi pamoja na walimu kuwa wayatunze majengo hayo ili yaweza kukaa kwa muda mrefu na kusaidia watoto wengine huko mbeleni sanjali na kuwataka wananchi wote wa kijiji cha Ifwagi kukaribia katika tawi la TPB lililopo Mafinga mjini kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kibenki kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Benki ya Tpb ,Diana Mnyonga ,aliyeketi wa tatu kulia katika Picha ya Pamoa na Baadhi ya viongozi wa Shule ya Msingi Ifwagi na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi wa majengo ya vyoo yenye matundu 20 , Julai 05 Mwaka huu.
Muonekano wa Majengo ya Kisasa ya vyoo yenye matundu 20 yaliyojengwa kwa msaada wa benki ya Tpb katika shule ya Ifwagi Halmashauri ya Mufundi Mkoani Iringa Julai 05,mwaka huu.

Akipokea Msaada wa Majengo hayo Mwalimu wa shule hiyo, Bi Imani Nyoni amesema kwa muda mrefu walikuwa wakijaribu kuomba wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya wanafunzi pamoja na walimu pasipokupata mafanikio hivyo kukabidhiwa majengo hayo na Tpb ni faraja kubwa kwao..

Amesema Shule hiyo ya Ifwagi ina jumla ya wananfunzi 211 ambao ni idadi kubwa ya wanafunzi na kulikuwa na uhaba wa matundu ya vyoo hali ambayo ilipelekea baadhi ya wananfunzi kujisaidia nje ya shule hiyo ameishukuru Tpb kwa kuondoa changamoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news