Upatanishi mvutano wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance watua UN

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono juhudi za upatanishi za Umoja wa Afrika katika kutanzua mzozo wa bwawa kwenye Mto Nile kati ya Ethiopia Sudan na Misri.

Baada ya kikao cha Baraza la Usalama lilizitaka nchi hizo tatu kuanza tena majadiliano yao ambayo hadi hivi sasa hayajaweza kuleta mafanikio muhimu tangu yalipoanza karibu miaka 10 iliyopita.

Mkutano huo wa Baraza la Usalama uliitishwa na Misri na Sudan kutokana na kile walichokieleza ni kitisho muhimu kinachowakabili wananchi wa nchi hizo mbili kutokana na Bwawa la Ethiopia la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD).

Mvutano uliongezeka tangu Jumatatu baada ya Addis Ababa kutangaza imeanza awamu ya pili ya kujaza maji kwenye bwawa hilo.

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya nchi za Pembe ya Afrika, Parfait Onanga Anyanga aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba licha ya juhudi mbalimbali za upatanishi Ethiopia, Sudan na Misri

"Tuna amini kwa pamoja pamoja na washirika wenu kuna nafasi ya kusonga mbele katika kutanzua matatizo yanayohusiana na GERD kwa njia ya amani na maelewano,"amesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry amelitaka Baraza la Usalama kuzihimiza nchi hizo tatu kufikia makubaliano katika muda wa miezi sita ijayo juu ya matumizi ya maji ya Mto Nile.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Nishati wa Ethiopia, Seleshi Bekele Awulachew amesema, wanakabiliana na mradi wa kuzalisha umeme kwenye bwawa ambao si wa kwanza barani Afrika au kwingineko duniani.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan aliliambia baraza hilo kuwa, huu ni wakati wa kipekee kuwahi kutokea kwa bazara hilo kuchukua jukumu la kidiplomasia kuzuia mgogoro na wala si kupeleka walinda amani.

Mariam Sadiq al-Mahdi, Waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Sudan alieleza kuwa, "Lakini ni juhudi za kidiplomasia kuepusha mgogoro kwa kuzingatia ishara za awali na kuchukua hatua za mapema kujenga uaminifu, kujenga uaminifu katika jumuia muhimu sana ya kikanda kama Umoja wa Afrika. Pamoja na kujenga uaminifu kati ya nchi muhimu kama vile Sudan, Ethiopia na Misri,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news