Waziri Kalemani azindua Mradi wa PERI Urban Mwanza

Hafsa Omar na Veronica Simba-Mwanza

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amezindua Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban), Julai 9,2021.

Tukio hilo limefanyika, Julai 9, 2021, katika mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

Akizungumza na wananchi, amesema kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kuhakikisha kuwa inakwenda kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya pembezoni mwa jiji hilo.

Amefafanua kuwa, maeneo hayo wamechelewa kupata umeme kwakuwa hayakuwa na sifa ya kupata umeme wa 27,000 lakini kwasababu Serikali ni sikivu imeamua maeneo yote ya mjini yanayofanana na kijijini yapelekewe umeme kwa 27,000.
Wananchi wa mtaa wa Nyamwilolelwa, Kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(katikati) kabla ya kuwasha umeme kwenye zahanati ya mtaa huo, Julai 9,2021.

“Tulipoanza kusambaza umeme vijijini tukajikuta tumepeleka umeme mwingi vijijini maeneo mengi ya mijini tena yana sura sawa na vijijini hayakuwa na umeme lakini kwasasa kutokana na mradi huu maeneo yote kama haya yatapata umeme wa bei nafuu,”alisema.

Aidha, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anasambaza umeme katika maeneo yote ya mitaa hiyo ndani ya miezi 12 ili wananchi wa maeneo hayo waanze mara moja kupata huduma hiyo muhimu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwatambulisha kwa wananchi wakandarasi, Kampuni Namis Corporate Ltd wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban). Waziri alizundua mradi katika mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza, Julai 9,2021.

Ameongeza kuwa, kwakuwa eneo hilo nyumba zipo karibu,hivyo itakuwa rahisi kwa mkandarasi kukamilisha kazi hiyo kwa haraka na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo ili kazi ikamilike mapema.
Wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Ilemela, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa usambazaji umeme maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika Julai 9, 2021 Mgeni Rasmi akiwa ni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.

Amesema kuwa, Taasisi za umma zipewe kipaumbele kuunganishiwa na umeme kwakuwa maeneo hayo ni muhimu katika jamii na bila huduma hiyo hawataweza kutoa huduma bora.

Amesisitiza kuwa, wananchi wakikamilisha malipo ya kupata huduma ya umeme waunganishiwe na huduma hiyo ndani ya siku 14 ili wananchi hao waanza kutumia umeme kwa kujiletea maendeleo mbalimbali.
Wananchi wa mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza wakifurahiya uzinduzi Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban), Julai 9,2021.

Vilevile, amemtaka mkandarasi kutumia nguzo za zege kusambazia umeme kwakuwa zinadumu kwa muda mrefu na zitaondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwa tatizo la kuanguka kwa nguzo.
Mbunge wa jimbo la Ilemela, Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa amezindua wa Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban), Julai 9,2021.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Ilemela, Angeline Mabula, ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuleta mradi wa Peri Urban, kwani umekuwa mkombozi kwa wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuunganisha umeme huo majumbani na kutumia kwa shughuli za kiuchumi.

Naye, Meneja Miradi ya Umeme Vijijini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale, amesema mradi huo mkubwa unatarajia kuunganisha umeme wananchi zaidi ya 10,224.
Meneja Miradi ya Umeme Vijiji, Kanda ya Ziwa, Mhandisi Ernest Makale, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Igogwe, kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme awamu ya pili katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Mwanza (Peri Urban), Julai 9,2021.

Ameeleza kuwa, uhitaji wa umeme ni mkubwa lakini Serikali imejipanga na itahakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria kwa kuwasha kwa umeme katika zahanati Nyamwilolelwa iliyopo katika mtaa wa Nyamwilolelwa, Kata ya Chibula, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza, Julai 9,2021.

Dkt. Kalemani, pia amewasha umeme katika zahanati ya Nyamwilolelwa iliyopo katika mtaa wa Nyamwilolelwa, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news