WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI NCHINI MOROCCO KWA ZIARA YA KIKAZI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2021 amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.

Akiwasili katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli Alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mohammed V uliopo jijini Casablanca nchini Morroco, Julai 12, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mohammed V uliopo jijini Casablanca nchini Morroco, Julai 12, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mohamed V uliopo jijini Casablanca nchini Morroco, Julai 12, 2021.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news