ZEC yakabidhi Ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2020 kwa Rais Dkt.Mwinyi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi kwa watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa kufanikisha vyema Uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 28, mwaka 2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Uchanguzi Zanzibar Jaji Mstaaf Mhe.Hamid Mahmoud, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Julai 13, 2021 Ikulu Jijini Zanzibar mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kumkabidhi Rais Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa kumchagua Rais wa Zanzibar, kuwachagua Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Madiwani na kuvihusisha vyama 19 vya siasa.

Katika pongezi hizo, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kwamba kuna kila sababu ya kutoa pongezi kwa wadau wote wa uchaguzi wakiwemo tume husika, vyombo vya ulinzi na usalama, asasi za kiraia pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutoka na kwenda vyema kwa zoezi la uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

“Nachukua fursa hii ya pekee kutoa shukurani zangu za dhati kwa Tume ya Uchaguzi na wadau wote wa uchaguzi kutokana na zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,2020 kwenda vyema,”amesema Dkt.Mwinyi.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inafanya kila liwezekanalo ili kuepuka changamoto zisije kutokea tena katika chaguzi zijazo kwani lengo la Serikali ni kuzifanyia kazi changamoto zilizopo.

Amesisitiza kwamba, mafanikio makubwa yameweza kupatikana katika zoezi hilo kutokana na Tume hiyo kwenda na wakati kwa kutumia mfumo mpya wa uandikishaji wa kisasa wa TEHAMA.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi ametoa pongezi zake kwa tume hiyo kwa kufanikisha kuchapisha kura zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu hapa hapa Zanzibar na sanjari na kukamilisha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya Uchaguzi ndani ya saa 24 baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa pongezi kwa tume hiyo ya Uchaguzi kwa kazi kuwa iliyofanya ikiwa ni pamoja na kukabidhisha ripoti hiyo huku akisisitiza kwamba juhudi za makusudi zitachukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kwamba changuzi zijazo zinakuwa bora zaidi.

Mapema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kabla ya kumkabidhi Rais Dkt. Mwinyi ripoti hiyo, alimueleza kwamba ripoti hiyo imegawanyika katika sura saba na imezingatia hatua za mzunguko mzima wa uchaguzi hivyo imezingatia hali ilivyokuwa kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Mwenyekiti hiuyo wa Tume ya Uchaguzi ametoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Mapainduzi ya Zanzibar kwa kuweza kugharamia Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2020 kwa kiwango cha asilimia mia moja ya gharama zote za uchaguzi na fedha zote hizo kupatikana kwa wakati muwafaka.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mstaaf Mhe. Hamid Mahmoud (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Jijni Zanzibar kukabidhi Ripoti ya Uchaguzi Mku wa Zanzibar ulifanyika Oktoba,28, 2020. mwaka jana.

Amesema kuwa, hatua hiyo ya Serikali ndiyo iliyowezesha tume hiyo ya uchaguzi kuendesha na kusimamia uchaguzi huo kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Aidha, Mwenyekiti huyo ametoa shukurani kwa viongozi na watu wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, jambo lililopelekea uchaguzi huo kuonekana kuwa huru na wa haki.

Jaji Hamid pia, alimueleza Rais Dkt. Mwinyi kwamba uchaguzi huo Mkuu wa 2020 ulifanyika kama ulivyopangwa bila ya kutokezea hitilafu yeyote iliyosababisha kurejewa au kufunguliwa mashtaka ya kupinga matokeo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jaji Mstaaf Hamid Mahmoud.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Amesema kuwa, kura ya mapema iliweza kufanyika kwa mara ya kwanza na iliwarahisishia walengwa waliotajwa katika sheria ya uchaguzi kufanya kazi siku ya uchaguzi wa pamoja kwa ufanisi zaidi.

Amesema kwamba, tume imeweza kuwapata wataalamu wazawa waliofanikiwa kutengeneza mfumo mpya wa uandikishaji wa kisasa wa TEHAMA pamoja na kutayarisha mifumo mingine ya uchaguzi iliyoiwezesha tume kutekeleza zoezi la uchaguzi kwa usiri na kwa ufanisi bila ya kuingiliwa.Mwenyekiti huyo wa tume alimueleza Rais Dkt. Mwinyi kwamba tume imeweza kuchapisha kura zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu hapa hapa Zanzibar na kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar tume imeweza kukamilisha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya Uchaguzi ndani ya saa 24 baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe.Jaji Mstaaf Hamid Mahmoud,(kulia kwa Rais) akiwasilisha Ripoti ya Uchanguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika mwaka jana Oktoba 28,2020, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi ambaye alifuatana na Wajumbe wake pia, alitumia fursa hiyo kumueleza Rais Dkt. Mwinyi baadhi ya changamoto ambazo tume ilizikabili katika zoezi zima la Uchaguzi huo wa Oktoba 28, 2020.

Kutokana na maelezo ya Mwenyekiti huyo wa Tume kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha sheria ya kuanzisha Ofisi ya Tume ya Uchaguzi namba 1 ya mwaka 2017, kila unapomalizika Uchaguzi Mkuu, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inatakiwa kutayarisha ripoti na kuiwasilisha kwa rais ndani ya miezi 12.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news