Ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Mary Masanja wilayani Mkuranga

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa ushauri kuhusu namna ya ugawaji miti kwa vikundi na taasisi mbalimbali alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Mkuranga. Kulia ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo na kushoto ni Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Mkuranga Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Charles Kaselya (kushoto).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Mkuranga alipofanya ziara leo, ambapo amewataka kubuni mbinu mpya za kuongeza idadi ya watalii katika eneo la misitu wanalomiliki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwa ameongozana na Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo kukagua eneo lililopandwa miche ya miti iliyo kwenye Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Mkuranga alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo.Wengine ni baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Mkuranga wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Charles Kaselya (kushoto) akitoa maelezo ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb)(katikati) leo Wilaya ya Mkuranga. Kulia ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mary Masanja (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Wilaya ya Mkuranga. Wengine ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof.Dos Santos Silayo (katikati) na Mhifadhi wa Misitu Wilaya ya Mkuranga Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Charles Kaselya (wa pili kulia).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news