Alex Msama arudi tena mjini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Msama amefunguka kuwa baada ya ukimya mrefu wa takribani miaka sita wa kutoandaa matamasha ya burudani wanatarajia kufanya tamasha kubwa la nyimbo za injili Oktoba 3, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
Mmoja wa Waimbaji nyota wa muziki wa injili Upendo Nkone (wa tatu kulia) akiimba kwa hisia moja ya wimbo wake mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha kubwa la Kumshukuru Mungu litakaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promosheni,Oktoba 3,2021 katika uwanja wa Uhuru,Kulia ni Mwimbaji mwingine mahiri aitwaye Mess Chengula na kushoto ni Jessica Honole.

Msama ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema tamasha hilo litakua la kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo amelivusha salama Taifa la Tanzania katika mambo magumu ambayo imepitia.

Msama amesema kuwa tamasha hilo litakua limebeba mambo mengi ambapo kadri siku zitakavyokua zinasonga mbele ndivyo ambavyo watakua wakieleza zaidi juu ya mambo ambayo yatafanyika siku hiyo.

"Tamasha hili litakua la kihistoria kwa sababu hatujafanya takribani miaka sita, niwaambie mashabiki wote waliomiss matamasha yetu kuwa tunarejea kwa nguvu kubwa na tutahakikisha kila ambaye atalipa kiingilio chake atapata burudani ya kutosha.

Kutakua na wasanii tofauti tofauti, wa ndani ya Nchi na wa nje ya Nchi, tutaalika waimbaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kila mmoja anafurahia tamasha letu," Amesema Msama.

Amesema utofauti mwingine wa tamasha hili ni kwamba halitofanyika Dar es Salaam pekee bali wamepanga lifanyike kwenye Mikoa mingine nane ili kutoa fursa kwa mashabiki na watanzania walioko nje ya Dar es Salaam kuhudhuria.

Kwa upande wake msanii wa injili nchini, Jessica Honole amesema wao kama wasanii wanamshukuru Mungu kwa kuwezesha kurudi kwa tamasha hilo tena kwani tamasha hilo limekua ni baraka kwenye maisha yao.

" Hakika tunamshukuru Mungu kurejea kwa matamasha haya, yamekua ni chachu kwa wasanii wengi wa injli nchini lakini zaidi yameokoa maisha ya wengi wapo waliobarikiwa na kuokoka kupitia matamasha ya Msama hivyo niwasihi watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Oktoba 3 pale Uwanja wa Uhuru," Amesema Jesca.

Nae nguli wa muziki wa injili, Upendo Nkone amethibitisha kushiriki tamasha hilo ambapo amewaomba watanzania wote bila kujali tofauti zao kujitokeza kwa wingi kumshukuru Mungu kupitia tamasha hilo.

"Ni muda mrefu hatujafanya matamasha haya ya shukrani, hivyo naamini Oktoba 3 tutakuja kitofauti na hakika burudani itakuepo ya kutosha hivyo watanzania na mashabiki zetu kwa ujumla wasikose," amesema Nkone.

Mess Chengula nae ni mmojawapo wa wasanii ambao wamethibitisha ushiriki wao na kutoa wito kwa watanzania wote kujitokeza katika Uwanja wa Uhuru kushuhudia kurejea kwa tamasha hilo pamoja na kupata burudani ya aina yake.

MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news