Aliyewahi kuwa Bosi wa ATCL, David Mataka na wenzake wahukumiwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka kulipa faini ya Shilingi milioni nane au kutumikia kifungo cha miaka minne jela.
Ni baada ya kupatikana na hati ya makosa manne yaliyokuwa yakimkabili.

Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 20, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili hukumu.

Mataka amekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara Serikali ya Shilingi Bilioni 71.

Aidha, mbali na Mataka, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu, Dkt. Ramadhan Mlinga na aliyekuwa Mwanasheria wa PPRA , Bertha Soka, ambao wamehukumiwa kulipa faini ya Shilingi milioni Mbili kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja.

Ni baada ya kupatikana na hatia ya katika shitaka moja la kughushi mhutasari wa kikao.

Dkt.Mlinga na Soka walidaiwa kuwa Machi 19, 2008 katika ofisi za PPRA Ilala, Dar es Salaam walighushi muhtasari wa kikao wa tarehe hiyo, wakionesha kwamba mamlaka hiyo ilikaa kikao na kujadili maombi ya kuidhinisha ATCL ikodishe ndege aina ya Airbus.

Mkataba ambao unadaiwa kuisababishia serikali hasara kubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news