DC GEITA: SANAA IWE FURSA YA AJIRA

Na Robert Kalokola,Geita

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amewata wasanii katika Wilaya ya Geita kutumia vipaji vyao kutengeneza fursa za ajira kwa kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi na jamii ili kuweza kusaidia jamii inayowazunguka na kuajiri watu wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya Kosa la Mama iliyochezwa na wasanii wa Geita chini ya Mkurugenzi wao Maiko Kapaya. (Picha na Robert Kalokola).

Amesema hayo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Kapaya Film, Maiko Kapaya iliyofanyika katika Ukumbi wa Desire Park ikiwa ni uzinduzi wa filamu yake mpya iliyochezwa na wasanii wa Wilaya Geita ikijulikana kwa jina la Kosa la Mama.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema wilayani humo itafanya jitihada za kusaidia wasanii katika Wilaya hiyo ili waweze kukuza sanaa na vipaji vyao na kuweza kuajiri watu wengine.

Katika kuendelea kuwainua vijana kiuchumi kupitia sanaa ya uigizaji nchini ili kuwawezesha kujiajiri na kutengenzea ajira kwa wengine mkoani Geita,Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema wako tayari kuwaisaidia vijana wa sanaa hiyo katika kuwapa kipaumbelea kwenye mikopo inatolewa na halmashauri zote za wilaya hiyo ili kuhakikisha vijana wanaitumia sanaa kama ajira.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo akionyesha CD ya Maigizo iliyozinduliwa rasmi katika ukumbi wa Desire park iliyochezwa na Wasanii wa Geita chini ya Mkurugenzi wa Kapaya film,Maiko Kapaya ( Picha na Robert Kalokola).

Mkuu wa Wilaya Geita katika kuunga mkono jitihada za kukuza na kuinua sanaa kwa wasanii wa Wilaya ya Geita amewachangia Kapaya Film kiasi cha milioni moja ili kuweza kuendeleza kazi hiyo kwa ubora zaidi.

Katika risala yake kwa Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alikuwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya Kapaya aliomba serikali isaidie upatikanaji wa kiwanja chenye ukumbwa wa Ekari 7 ambazo zitasaidia mipango yake ya mbeleni ya kujenga na kuanzisha kituo cha kulea watoto yatima.

Aidha, Mkuu wa Wilaya Wilson Shimo amewataka wasanii wote katika Wilaya hiyo ikiwa ni wacheza ngoma,muziki,maigizo na mengine kushiriki katika shughuli mbalimbali za serikali kama za mbio za mwenge.
Mkurugenzi wa Kapaya Film ambaye ndiye msimamizi wa filamu ya Kosa la mama iliyozinduliwa rasmi na mkuu wa Wilaya ya Geita Wilson Shimo (Picha na Robert Kalokola).

Maiko Kapaya ni mkurugenzi wa Kampuni ya Kapaya Film ambayo imezindua filmu mpya ya maizigo yenye jina la Kosa la Mama ambayo anasema ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuongeza umakini katika jamii hasa malezi ya Mama kwa watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news