KAMATI YAPENDEKEZA JERRY SILAA AVULIWE UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa amepewa adhabu ya kuvuliwa Ujumbe wa Bunge la Afrika (PAP) na kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge.
Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa ripoti yake leo Agosti 31,2021 Bungeni jijini Dodoma kuhusu shauri la Mbunge huyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili, Emmanuel Mwakasaka amewasilisha ripoti hiyo mbele ya Bunge.

“Azimio la Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuhusu hatua za kuchukua kwa Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa kusema uongo kwamba mishahara ya Wabunge haikatwi kodi.

"Akiwa mbele ya Kamati hakukiri wala kujutia makosa yake hivyo kamati imemtia hatiani hivyo Bunge linaazimia Silaa asihudhurie mikutano miwili mfululizo na aondolewe kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP),"amesema.

Adhabu hiyo imekuja baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kujiridhisha kuwa alitoa kauli ya uongo kuhusu Mishahara ya Wabunge kutokatwa kodi

Aidha, wakati wa kusikiliza shauri lake, Jerry alionekana kutojibu maswali kama ilivyopaswa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news