Maajabu ya TARURA kuwafikisha Watanzania kusikofikika yawagusa wengi


Chini ni sehemu ya kazi bora zaidi za ujenzi wa madaraja na barabara ikiwa ni kazi inayofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA);

Hivi karibuni, Serikali ilizindua Mpango Mkakati wa Pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wenye thamani ya shilingi Trilioni 3.6.
 
Akizindua mpango huo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Ummy Mwalimu amebainisha namna Serikali itakavyoimarisha utendaji kazi wa wakala huo kwa kuwapa magari na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo wahandisi.

Uzinduzi wa mpango huo ulioenda sambamba na uzinduzi wa kauli mbiu isemayo ‘TARURA tunakufungulia barabara, kufika kusikofikika’, Waziri Ummy amesema utekelezaji wa mpango huo utaleta mapinduzi makubwa ya ujenzi wa barabara nchini na kurahisisha maeneo ya mijini na vijijini kufikika.

“Mpango huu unaanza mwaka huu 2021/22 hadi 2025/26 na utaongeza mtandao wa barabara kutoka kilometa 2,404.90 hadi 3,855.65, changarawe kutoka kilometa 29,116.57 hadi 102,358.14 na madaraja kutoka 2,812 hadi 6,620 na fedha zitakazotumika ni Sh.Trilioni 3.6,”amesema.

Ameseza kuwa, kama mpango mkakati huo utatekelezwa vyema zitajengwa barabara za changarawe kilometa 73,242 na kwamba hayo ni mafanikio makubwa kwa kuwa asilimia 70 ya barabara nchini ni za vumbi.

Post a Comment

0 Comments