Mwandishi wa Ayo Tv afariki kwa ajali

NA MWANDISHI MAALUM

Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.
Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery,”ameandika Ayo.

“Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri,"ameongeza.

Uongozi wa Diramakini Blog unawapa pole ndugu, jamaa na marafiki ukiwemo uongozi wa Ayo Tv kwa kuondokewa na mtu wao muhimu katika tasnia ya habari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news