Rais Samia aanza kurekodi kipindi cha Royal Tour kuitangaza Tanzania kimataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijumuika pamoja na Wananchi mbalimbali Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, alipokua akianza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Msanii Mkongwe wa Taarab Asilia Nchini Bibi Mariam Hamdani, alipokutana nae katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,2021, kabla ya kuanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, wakati wa kuanza kurekodi rasmi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Zanzibar leo Agosti 29,202. PICHA NA IKULU.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news