Rais Samia afanya teuzi zifuatazo leo Agosti 17,2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali  kama ifuatavyo:-

1.        Amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

 

2.     Amemteua Prof.  Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.  Kabla ya uteuzi huu Prof. Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (upande wa Mifugo)

Prof. Ole Gabriel anachukua nafasi ya Bw. Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu.  Prof. Ole Gabriel ataapishwa tarehe 21 Agosti, 2021, saa 03:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na Mabalozi Wateule watatu (03) kama ifuatavyo:-

1.     Balozi Mteule Lt. Jen. Yakub Hassan Mohamed kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

2.     Balozi Mteule Mahmoud Thabit Kombo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

3.     Balozi Mteule Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

 
Post a Comment

0 Comments