Rais Samia awasili jijini Zanzibar akitokea nchini Malawi katika Mkutano wa 41 wa kawaida SADC



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na kumpongeza Rais Mhe. Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili Zanzibar wakati akitokea nchini Malawi ambapo alishiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021. (PICHA NA IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news