Serikali ya Awamu ya Sita yakanyagia gia kasi ujenzi ghorofa za kisasa Mji wa Serikali Mtumba

NA MWANDISHI MAALUM

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba, Bwana Meshack Bandawe amekutana na wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa wizara zote ili kujadili maandalizi na utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za ghorofa za wizara zitakazojengwa awamu ya pili katika mji wa Serikali Dodoma.
Katibu wa kikosi kazi cha Taifa cha kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba Bwana Meshack Bandawe akiongoza Kikao cha wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara zote kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za ghorofa za wizara zitakazojengwa awamu ya pili katika mji wa Serikali.

Kikao hicho ni kufuatia maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyezitka Wizara kuanza taratibu za ujenzi wa ofisi za awamu ya pili baada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu na majengo ya ghorofa yatakayotumiwa na wizara mbalimbali katika mji wa Serikali Mtumba.

“Kwakuwa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara ndiyo timu ya ufundi ya usimamizi wa ujenzi na wasaidizi wa makatibu wakuu ni vyema tukajipanga kikamilifu ili kutekeleza ujenzi kwa tija, ufanisi, ubora, muda, kanuni, taratibu na kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa na Serikali” alisema bwana Bandawe katika kikao hicho.
Wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara zote wakiangalia wasilisho la michoro ya usanifu na ubunifu wa mji wa serikali na majengo ya wizara yatakayojengwa awamu ya pili katika mji huo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za ghorofa za wizara kilichofanyika Mtumba Dodoma.
Katibu wa kikosi kazi cha Taifa cha kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba Bwana Meshack Bandawe akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara zote baada ya kikao cha kujadili utekelezaji wa ujenzi wa ofisi za ghorofa za wizara zitakazojengwa awamu ya pili katika mji wa Serikali.

Kwa mujibu wa bwana Bandawe, kikao hicho pia ni maandalizi ya vikao vitakavyofuata vya makatibu wakuu na mawaziri kwa ajili ya kupokea maagizo na maelekezo ya Serikali katika kutekeleza shughuli za ujenzi kwa ufanisi.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mji wa Serikali ilikamilika Aprili, 2019 na kuwezesha Wizara na taasisi mbalimbali kuhamishia ofisi zake mkoani Dodoma ambapo ujenzi wa awamu ya pili ya mji huo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzai sasa baada ya Serikali kutoa pesa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news