Spika Ndugai awaomba radhi Wakristo, Watanzania wote kwa kauli yake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amewaomba radhi Wakristo na Watanzania wote kwa ujumla waliokwazika na kauli yake aliyoitoa leo asubuhi bungeni akielezea mstari wa Biblia.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai

Hayo yamebainishwa leo Agosti 31, 2021 kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoonwa na DIRAMAKINI Blog, alichokuwa anamaanisha Mheshimiwa Spika ni kwamba, "Yusufu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda mpaka Yerusalemu kuhesabiwa" na si Yesu kama alivyotamka.

"Kilichotokea ni hali ya kibinadamu ya ulimi kuteleza ambayo inaweza kumtokea mtu yeyote,"imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments