Tanzania yajazwa Trilioni 2.7/- kutoka Benki ya Dunia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick, wakisaini mmoja kati ya mikataba mitano ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar, tukio ambalo limefanyika, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick ndio waliosaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).

Kupitia mkopo huo, miradi itakayotekelezwa ni katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.

Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.

Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news