Vilio,simanzi zatawala kuagwa miili ya wafanyakazi watano wa TRA waliofariki kwa ajali

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Miili ya wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato (TRA) waliofariki kwa ajali ya gari jana imeagwa, huku simanzi ikiwa imetawala miongoni mwa waombolezaji, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.
Wafanyakazi hao walifariki baada ya gari walilokuwemo wakilitumia kufukuza gari lililosadikiwa kuwa na magendo kugonga kwa nyuma Fuso.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi, ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Tunduma- Mbeya katika kijiji cha Hanseketwa saa 11:45 alfajiri.

Wafanyakazi wanne walikuwa wa Mkoa wa Mbeya na mmoja wa Tunduma mkoani Songwe na walikuwa katika doria na walihisi gari moja kupakia mzigo wa magendo na kuamua kulifukuza.

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafanyakazi wake watano waliofariki kwenye ajali ya gari eneo la Old Vwawa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wakiwa wanalikimbiza gari ambalo lilidhaniwa kuwa na bidhaa za magendo.

"Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa majonzi na masikitiko makubwa natoa taarifa ya vifo vya Maofisa watano waliokua Watumishi katika Idara ya Ushuru na Forodha vilivyotokana na ajali mbaya ya gari alfajiri Augut 23 2021, waliofariki ni Benard Balagi Mushingi (40) Afisa Forodha (TRA Songwe).

"Wengine ni Azaria Asakwe Sivonike (42) Dereva TRA Mbeya, Joel Isaya Mitondwa (36) Afisa Forodha TRA Mbeya, Said Mrisho Buddy (34) Afisa Forodha TRA Mbeya na Fahad Hassan Haji (26) Afisa Forodha Msaidizi TRA Mbeya.

"Familia ya TRA itaendelea kuwakumbuka Marehemu wote watano na kuenzi mchango wao katika kazi ya kukusanya mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, sisi Watumishi wenzao vifo hivi vimetuacha na simanzi kubwa na pengo lisilozibika kirahisi kwa nguvu kazi tuliyoipoteza pamoja na kuzingatia maarifa na weledi waliokuwa nao,"ameeleza Kamishna Mkuu TRA, Alphayo Kidata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news