Waziri aagiza Mbunge Askofu Gwajima akamatwe upotoshaji chanjo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mheshimiwa Dkt.Doroth Gwajima ambaye ni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( TAKUKURU) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima.
Ni ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko-19 inayotolewa hapa nchini.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Awali akizungumzia kuhusiana na Chanjo ya (Uviko-19) Waziri Gwajima amewataka Watanzania kujitokeza kuchanja kwani chanjo ni salama kabisa na kwamba uzushi wowote unaozushwa juu ya chanjo unapswa kupuuzwa akapongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara chini ya Mganga Mfawidhi Dkt. Joachim Eyembe kwa kazi nzuri wanayofanya kuhudumia wananchi kwa ufanisi.

Akawataka watumishi wa afya mkoani Mara na Tanzania kwa ujumla, kutoa elimu ya corona na kuhimiza Wananchi kuchanja.

"Watu wengi wanaolazwa na kutumia Oxygen ni wale ambao hawajachanja, chanjo ni salama, uzushi na upotoshaji unaotolewa upuuzwe.

"Mtu anakataa chanjo ya Uviko-19 lakini anatumia dawa za TB na mipira ya Kondomu ananunua wakati hatuna kiwanda. hizi zote zinatolewa nje, kwa hiyo chanjo ni salama kabisa hata Rais Hayati Magufuli watu hawakumuelewa alisema tusikimbilie chanjo bali tujiridhishe na serikali ya Awamu ya Sita imejiridhisha tayari na ndio maana imeruhusu chanjo ambayo ni Salama kabisa Wananchi tuepukeni uzushi na upotoshwaji juu ya chanjo. Chanjo zilikuwepo na zitakuwepo vinginevyo tungekuwa vilema na viwete Kutokana na polio na surua," amesema Waziri Gwajima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news