Waziri Mkuu aomboleza kifo cha Mwalimu Kashasha

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wapenzi wa soka nchini kutokana na kifo cha mchambuzi maarufu wa soka, Mwalimu Alex Kashasha (64) kilichotokea wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa. (Picha na Maktaba).

Mwalimu Kashasha ambaye alifikwa na umauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki, alikuwa mchambuzi mahiri wa mchezo wa soka kwenye televisheni ya Taifa (TBC1).

“Atakumbukwa kwa ustadi wake wa kuchambua mechi za soka mubashara pamoja na vipindi vya maelezo ya mechi za soka za ndani na nje ya nchi,” amesema Waziri Mkuu.

“Ninawaomba wanafamilia na wapenzi wa michezo tuendelee kumuombea ili apumzike kwa amani. Tutaendelea kuenzi mchango wake katika kukuza vipaji vya michezo hapa nchini.

“Mwalimu Kashasha ambaye alikuwa ni kati ya walimu wazuri wa mchezo wa soka nchini, ameacha pengo kubwa kwenye tasnia ya michezo kama mwalimu na kwa watu wengi waliopita kwenye mikono yake,” amesema Waziri Mkuu. 

Amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news