FCS yazitaka Asasi za Kiraia Tanzania kushikamana kwa pamoja

NA MWANDISHI MAALUM

Asasi za Kiraia nchini zimetakiwa kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika taasisi zao ili ziweze kufahamika kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
Pia zimetakiwa kuhakikisha zinaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndio miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati mpya wa Foundation For Civil Society (FCS) Rais wa taasisi hiyo, Dkt.Stigmata Tenga amesema kuwa, asasi  za Kiraia zinapaswa kujengwa kutokana kuwa ni muhimili mkubwa wa maendeleo nchini na kwamba wananchi wanapaswa kuzifahamu.
Rais wa FCS, Dkt. Stigimana Tenga akizungumzia mpango huo mara baada ya kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

“Tuisemee sekta hii na yale yote ambayo sekta hii inayafanya kwenye jamii, yasemeeni mnayoyafanya ili yajulikane msione aibu yeyote,”alisema Dkt.Tenga.

Aliongeza kuwa, asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa hilo ndio lengo kubwa la FCS katika Dira yake.

“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujali kuna nini, bali kuwashirikisha wenzetu matatizo ambayo sekta ya asasi za kiraia nchini inapitia ambayo yanahitaji kutatuliwa kwani ni matatizo yanayojikita katika mifumo,” aliongeza Dkt.Tenga.
Mkurugenzi wa FCS, Francis Kiwanga (wa tatu kulia) akiwa na Rais wa taasisi hiyo, Dkt. Stigimana Tenga (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya FCS,Dkt. Richard Samabiga (wa kwanza kulia) wakiangalia mpango mkakati utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa mpango huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za FCS jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, akielezea namna ambavyo FCS itavyotekeleza majukumu yake katika kuusimamia mpango huo.

Aidha, alisema hawapaswi kutatua matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.

“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika asasi,” alisema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga alisema kuwa wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS
ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.
Alisema, kupitia mpango huo taasisi yao itaendelea kufanya kazi na asasi mbalimbali za kiraia ambao ndio wadau wao muhimu katika kuwafikia wananchi.

Alisema, falsafa ya taasisi yao inaamini kuwa umasikini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.

Alisema, katika rasilimali zao takribani asilimia 90 inakwenda vijijini kuhudumia wananchi.

“Rasilimali zetu tunavyogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini, tunaamini waliopo Dar es Salaam,taasisi nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani,kuliko waliopo vijijini,"alisema Kiwanga.
Baadhi ya watumishi wa FCS na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa katika mpango kazi wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili na kuwaheshimu kwani wao ndio wabia wao wakubwa na kwamba sauti yao ina ukubwa wa kuweza kuwafikia wananchi wengi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa NGOs, Dkt.Richard Sambaiga aliipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.

Alisema, mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.

Mpango mkakati huo umejikita katika kutekeleza miradi ya utawala bora, usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu, kukuza uchumi na kujenga amani na utatuzi wa migogoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news