IGP Sirro afanya mabadiliko makamanda wa polisi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo ya makamanda wa Polisi wa mikoa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa polisi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa, Kamishna msaidizi wa Polisi, ACP Revocatus Malimi amehamishwa kutoka mkoa wa Kagera kwenda makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Aidha,nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi waPolisi, ACP Awadhi Juma Haji.

Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Omary Said Nassiri amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi.

Post a Comment

0 Comments