KATELE AENDELEA KUPETA, ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA WANAWAKE TUGHE TAIFA

Na Rotary Haule,Dodoma

WAJUMBE wa Kamati ya Wanawake ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (Tughe) wamemchagua, Catherine Katele kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo kwa ngazi ya Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake ya Tughe Taifa, Catherine Katele akizungumza jambo baada ya kuchaguliwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dodoma. (Picha na Rotary Haule).

Katele, amechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dodoma baada ya kupata kura 91 dhidi ya mpinzani wake Lidya Butalimbo aliyepata kura 19 dhidi ya wajumbe halali 110.

Katele,amepata ushindi wa kishindo kutokana na ustadi wake wa kujieleza na hata kujibu kwa ufasaha maswali aliyoulizwa mbele ya wajumbe wakati wa kujinadi.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi, Andrew Mwalwisi, amesema kwa mujibu wa kura alizopata Katele zimempa fursa ya kumtangaza kuwa mwenyekiti wa Taifa wa kamati ya Wanawake wa Tughe.

"Kwa mamlaka niliyopewa ya kusimamia uchaguzi huu wa Wanawake wa Tughe Taifa,napenda kumtangaza Catherine Katele kuwa mwenyekiti wa kamati ya Wanawake ya Tughe Taifa kwakuwa ameongoza kwa kupata kura 91 dhidi ya 19 za Butalimbo," amesema Mwalwisi.

Aidha, nafasi ya Katibu wa Wanawake kulikuwa na mchuano mkubwa kwa wagombea watatu akiwemo Lidya Butalimbo, Beatrice Masasi na Elizabeth Salikoki lakini hatahivyo uchaguzi huo ulirudiwa kutokana na mshindi kushindwa kupata kura zaidi ya nusu.

Katika uchaguzi wa awali Salikoki alipata kura 44 ,Masasi alipata kura 38 na Butalimbo alipata kura 28 na kwamba katika uchaguzi wa marudio waliochuana ni kati ya Salikoki na Masasi lakini Salikoki alipata ushindi kwa kupata kura 78 na Masasi kura 38.

Akizungumza na wajumbe hao mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Taifa Katele, amewashukuru wajumbe kwakuwa wamemuazima imani iliyopitiliza.

Katele, alisema pamoja na shukrani hizo lakini pia ameelekeza pongezi zake kwa Katibu Mkuu wa Tughe Hery Mkunda kwa jinsi alivyomnoa kuwa kiongozi.

Alisema kuwa,kwasasa uchaguzi umekwisha na hakuna nongwa tena kwakuwa waliomchagua na wasio mchagua ni kitu kimoja na kilichobaki ni kuwa wamoja katika kukiimarisha chama.

Katele, aliongeza kuwa ataitendea haki nafasi hiyo kwakuwa anatambua changamoto za Wanawake na kamwe hatowaangusha huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wajumbe hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news