🔴LIVE: Serikali yalifungia Gazeti la Raia Mwema

 

"Kwa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 9(b) cha Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya 2016 nimeamua kusitisha kwa muda wa siku thelathini (30) leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la Raia Mwema kuanzia kesho tarehe 6 Septemba, 2021.

"Uamuzi wa kusitisha leseni ya gazeti la Raia Mwema unatokana na mwenendo na mtindo wa uandishi wa habari na makala ambao kwa kiasi kikubwa unakiuka misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa kufanya upotoshaji wa mara kwa mara wa taarifa na uchochezi wa bayana

"Kwa kufanya hivyo gazeti hili limekiuka masharti ya leseni liliyopewa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuleta chuki miongoni mwa jamii na vilevile kuwafanya wananchi waichukie Serikali na viongozi wake," Gerson Msigwa, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news